Na Lucas Myovela_ Arusha.

Kamishina Mkuu wa TRA, Bw, Alphayo Kidata Akizungumza na wadau wa Kodi Jijini Arusha katika kikao kilicho wakutanisha wadau wa kodi na TRA ili kujadili mambo mbali mbali ya ulipaji kodi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku moja kamishna mkuu wa TRA Alphayo Kidata alisema unalengo la kurahisisha ulipaji kodi ili kuchochea maendeleo kupitia mapato.


"Mwelekeo wa serikali ni kulipa kodi bila shuruti hivyo kikao cha TRA na wadau wa kodi mkoa wa Arusha tunataka kuwasikiliza na kutatua kero zao lakini pia kutambulisha mifumo mbalimbali ya kielektroniki ili kurahisisha zoezi la ulipaji kodi" alisema Kamishna.


Alitaja mifumo hiyo kama  E - Filing kwa ajili ya return za biashara, kuimarisha upatikanaji wa mashine za EFD lakini pia kuangalia namna ya kureplace zile zilizoharibika.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela aliyefungua mkutano huo alisema TRA wametumia njia bora ya kuwasikiliza walipakodi kwani itaondoa mkimbizano.

"Hata sisi mkoa tumeanza kukutana na makundi ya sekta mbalimbali na wiki ijayo wataanza na sekta ya kilimo cha maua na mbogamboga kwa muda wa siku tatu na mamlaka zote zitakuwepo kwa lengo la kupata majibu ya matatizo yanayokabili sekta hiyo na kwa kero zitakazoshindikana zitapelekwe ngazi ya juu" alisema.

Naye Kelvin Remed meneja mazingira TAHA alisema hii ni fursa kwa walipakodi kukaa na viongozi wa ngazi ya juu ya TRA ili kufikisha kero zao moja kwa moja lakini pia kutoa ushauri wa namna bora kazi ya ukusanyaji kodi itafanyika.

"Tunaamini kukutana huku ni ili kuondoa mfumo wa kushurutishana na kutengeneza namna bora ya kila mmoja kutimiza wajibu wake hasa ukizingatia sekta nyingi zilikumbwa na changamoto ya Covid hivyo tunaweza kusonga mbele kwa pamoja".

Share To:

Post A Comment: