Monday, 26 July 2021

RC TABORA AAGIZA WANAOCHOMA MOTO KUKAMATWA

 

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kulia) akiangalia leo mmoja ya mahindi ambayo yamezalishwa na Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kwa ajili ya mbegu bora. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi Dkt . Emmanuel Mrema

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kushoto) akiangalia leo kili mbili za mbegu bora ya mahindi yaliyozalishwa na Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kwa ajili ya mbegu bora. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi Dkt . Emmanuel Mrema

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi Dkt . Emmanuel Mrema(kushoto) akimwonyesha leo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kulia) miche ya michikichi ambayo imezalishwa na Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kwa ajili ya mbegu bora.

 


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa wanawakamata watu watakaobainika kuchoma moto na kusababisha uharibifu katika mistu ya kupanda na ile ya asili katika maeneo mbalimbali.

Hali imekuwa ikisababisha hasara kubwa kwenye mistu na mimea ya Taasisi na watu binafsi.

Balozi Dkt. Batilda alitoa agizo hilo leo wakati akipokuwa na ziara ya kikazi katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) iliyokuwa na lengo la kuwahamasisha kuzalisha kwa wingi mbegu bora za Alizeti.

Amesema tabia ya uchomaji moto ovyo katika maeneo yote ya Mkoa wa Tabora kwa kisingizio cha kuandaa mashamba na wengine kutaka majani mapya yaote kwa ajili ya mifugo haikubaliki.

Balozi Dkt. Batilda amewataka Wakuu wa Wilaya zote na Watendaji kuhakikisha wanawakamata na kuchukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wenzake wenye tabia chafu ya kuchoma moto ya kuteketeza mistu na miti inayoendelea kupandwa.

Amesema ni vema Sheria Ndogo zilizopo zitumikea kuwaadhibu wale wote watakaokamatwa kwa makosa ya kuchoma mistu moto.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alilazimika kutoa agizo hilo haraka mara baada ya watu wasiofahamika kuchoma moto miti iliyokuwa imepanda katika barabara inayoelekea Chuo cha Musoma Utalii, eneo la Cheyo na eneo Malolo mjini Tabora.

Alisema kuwa haiwezekana mtu anachoma halafu viongozi wa mitaa au vitongoji wanasema hawawajui na kuongeza kuwa huo ni uzembe wa hali ya juu.

Bw. Mwanri alisema kuwa yeye atapambana na Mkuu wa Wilaya ambaye uharibifu utakea katika eneo lake na kushindwa kuwasimamia wa chini ili kukomesha tabia hiyo.

“Haiwezekani moto unachomwa katika maeneo yenu , mnashindwa kutambua mtu aliyeendesha hujuma hiyo…lazima panapotokea moto wahusika wasakwe na kuadhibu kwa mujibu wa Sheria” amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Amesema kuwa inasikitisha kuona wananchi na wadau mbalimbali wamejitokeza kupanda miti kwa wingi kisha wanatokea wachache wanachoma moto kwa kisingizio cha kusafisha mazingira au kutaka majani mapya kwa ajili ya mifugo.

Balozi Dkt. Batilda amesema wananchi lazima watambue miti ya asili na ile ya kupandwa ni kwa ajili ya faida ya wote na kuwaomba kusaidia kuwafichua watu wote wanaochoma miti kwa visingizio ambavyo sio vya msingi.

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi Dkt . Emmanuel Mrema amesema uchomaji wa moto ovyo katika eneo la Kituo umekuwa ukiwasababishia hasara kubwa katika mimea mbalimbali wanaendeshea utafiti.

Amesema katika siku za hivi karibu wamepata hasara ya kupoteza miche ya miti ya miembe ipatayo elfu 6 kutokana na watu wasiojulikana kuchoma moto.

Dtk. Mrema amemuomba Mkuu huyo wa Mkoa kusaidia katika utatuzi wa tatizo hilo amabalo limekuwa sugu Mkoani humo.

No comments:

Post a Comment