TUNAYAKUMBUKA MAISHA YAKE, TUNAENZI URITHI WAKE


NA BEATRICE SANGA-MAELEZO


Taasisi ya Benjamin William Mkapa kwa kushirikiana na Serikali imeandaa mdahalo wa kumbukizi ya maisha ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa katika ukumbi wa Mliman City Tarehe 14 July 2021.


Ameyasema hayo Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro, alipokutana na waandishi wa habari  katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 


Dkt. Senkoro amesema kauli mbiu katika mdahalo huo ni “ Hayati Benjamin Mkapa mwaka mmoja tangu atutoke, tunayakumbuka maisha yake, tunaenzi urithi wake” 


Mtendaji Mkuu ameongeza kuwa mgeni rasmi katika mdahalo huo atakuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na baadhi ya viongozi mashuhuri duniani ambao ni Rais wa 42 wa Marekani Mhe. Bill Clinton, aliyekuwa Waziri Mkuu wa uingereza Mhe. Tonny Blair, aliyekuwa Rais wa Nigeria Mhe. Olegesun Obasanjo na Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Ukimwi (UNAIDS), Winnie Byanyima ambao wote kwa pamoja watatoa  salaam zao kwa njia ya video wakielezea walivyomfahamu Hayati Benjamin Mkapa.


 “Mdahalo huu utalenga mchango wa hayati Benjamin mkapa ambao ameutoa katika taifa hili,na katika bara la  afrika na duniani kwa ujumla ambapo ni pamoja na Afya kwa wote ukiwa ni Urithi wa Rais Benjamin Mkapa katika kujenga Mifumo ya Afya imara na endelevu” amesema Dkt. Senkoro


Vilevile Wakati wa mdahalo huo Rais Samia atazindua mfuko maalum wa Taasisi “Endowment Fund”. Ambao unaanzishwa chini ya Taasisi hiyo wenye lengo la kuongeza chachu katika kuimarisha huduma za afya nchini.


Taasisi ya Benjamin William Mkapa ilianzishwa chini ya Sheria ya Uingizaji ya Wadhamini, Sura ya 375. iliyokusudia kuongeza na kusaidia juhudi za maendeleo za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo uzinduzi wa mpango wake wa kwanza ulijulikana kama "Programu ya Wenzake wa Mkapa" mnamo Julai 2005.


Hayati Benjamin Mkapa alifariki tarehe 23 Julai 2021 jijini Dar es salaam na kuzikwa nyumbani kwao kijiji cha Lupaso Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara.

Share To:

Post A Comment: