Wednesday, 21 July 2021

MAVUNDE AENDELEA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI NA KUZITAFUTIA UFUMBUZI ,AWEKA WAZI MIKAKATI YA MAENDELEO JIMBONI KWAKE

 


Day III :MTAA WA KIKOMBO MNADANI-KIKOMBO

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akiongozana na kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Dodoma Mjini jana amefanya mkutano wa kuwashukuru wananchi kuichagua CCM 2020 sambamba na kusikiliza kero na changamoto za wananchi.

Baada ya kusikiliza Changamoto za wananchi wa eneo husika,Mbunge Mavunde alieleza haya yafuatayo;

-Amewahakikishia Wananchi wa kata ya Kikombo juu ya kuanza kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuanzia njia panda ya Chamwino Ikulu mpaka makao ya makuu ya Jeshi.

-Uchimbaji wa kisima kipya cha Maji kwenye mtaa wa Chololo.

-Kuelekeza wataalamu wa Jiji wa Ardhi kupanga ratiba ya kwenda kuyatambua na kuwaonesha wananchi maeneo yao yaliyopimwa.

-Kurekebisha ramani ya eneo la wananchi lililoendelezwa ili kuepusha migogoro ya ardhi isiyo ya lazima.

-Ujenzi wa Nyumba ya Daktari katika zahanati ya Chololo kwa nguvu za wananchi,Diwani na Mbunge.

-Ujenzi wa shule ya Msingi Mpya mtaa wa Mnadani kwa nguvu za wananchi,Diwani na Mbunge.
No comments:

Post a Comment