Na Juma Mizungu,

Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe Jerry Silaa amezindua Shule ya Secondary Kipunguni. Kwa Mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Kata ya hiyo ya Kipunguni ndio imepata Secondary yake ya kwanza chini ya utawala wa Diwani Mhe. Stephen Mushi. Shule hiyo yenye Madarasa 10 ambayo yamejengwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam itapunguza kero ya watoto kusoma mbali na makazi yao.

Hafla ya Ufunguzi wa Secondary hiyo imefanyika katika Eneo ambalo Shule hiyo imejengwa maalufu kama "Bonde la Kikwete", Hafla hiyo ambayo ili hudhuliwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Madiwani wa Jiji la Dar es salaam wakiongozwa na Naibu Meya Jiji la Dar es salaam Mhe Saady Khimji.

Mhe. Saady Khimji Naibu Meya wa Jiji la Dar es salaam alieleza mpango wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kutaka kujenga madarasa ya ghorofa katika Shule hiyo ili kuendelea kupunguza matumizi ya Ardhi katika Eneo hilo pamoja na kuongeza vyumba vya kusomea kwa watoto.

Diwani wa Kata hiyo ya Kipunguni Mhe. Stephen Mushi alieleza kazi ambazo amezifanya tangu alipo apishwa kuwa Diwani wa Kata hiyo ikiwemo Ujenzi wa Shule ya Secondary Kipunguni madaasa 10,Ujenzi wa Matundu 15 ya Vyoo, Uchimbaji wa Kisima Kirefu, Ununuzi wa tofali 1,000 za ujenzi wa ofisi ya s/mtaa Kitinye, Uchimbaji wa Mfereji Emireti kwa kushirikiana na Wananchi pamoja na uboreshaji wa barabara za Kipunguni hasa sehemu korofi.

Aidha Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe Jerry Silaa alitoa pongeze kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa Ujenzi wa Shule hiyo ya Secondary lakini pia alieza mpango wake wa Ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Kipunguni pamoja na uboreshwaji wa barabara za Kipunguni ikiwemo barabara ya Moshi Bar Mombasa. Mhe Jerry aliendelea kwa kueleza mpango wake wa kufanya ziara ya kushukuru kila Kata na kuwaeleza Wananchi mpango wa Serikali katika kuleta maendeleo ya kila Kata katika Jimbo la Ukonga.

 




 

Share To:

Post A Comment: