Naibu Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Richard Kangalawe amewataka wanafunzi  wa Chuo hicho kuhakikisha wanapima afya zao, ili waweze kujikinga na kuwalinda wengine kutokana maambukizi ya virusii vya Ukimwi.



Akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya ukimwi ya Chuo hicho Dar es salam jana Prof. Kangalawe amesema kuna kila sababu ya wanafunzi kuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya UKIMWI ili wawe mabalozi wazuri kwa wengine.


“ Acheni tabia ya kupimana kwa macho badala yake kuweni na utaratibu wa kuwaona wataalamu wa afya ili kujua hali zenu, ili kuepuka unyanyapaa,” alisisistiza Prof. Kangalawe.



Kwa upande wake mratibu wa maadhimisho hayo ambaye pia ni mshauri wa wanafunzi Chuoni hapo Ukende Mkumbo amesema siku hii ni muhimu na ipo kimkakati hasa katika kupindi hiki ambacho wanafunzi wanaelekea kwenye mafunzo kwa vitendo (field) na likizo itawawezesha kujikinda, kuwalinda wengine na kusaidia serikali kuwa na nguvu kazi imara.


Afisa kutoka ofisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU ) Wilaya ya kigamboni Neema Kilongozi amesema Taasisi hiyo ina mahusiano ya moja kwa moja katika kupiga vita maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa wanafunzi  hususan rushwa ya ngono.


Nao baadhi ya wanafunzi wa Chuo hicho akiwemo Rais wa Serikali ya wanafunzi Godson Munisi na makamu wake Hafsa Sheturi wamesema mafunzo waliyoyapata kuhusiana na elimu ya UKIMWI ni Chachu katika nyanja mbalimbali za  kijamii, kisiasa, kiuchumi na itawawezesha kuwa mabalozi wazuri kwa kujikinga na kuwakinga wengine.


Imetolewa na;

Kitengo Cha Habari na Mahusiano

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

22.06.2021

Share To:

Post A Comment: