Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge, akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake fupi ya kukagua  Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Singida aliyoifanya juzi.

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandis Paskas Muragili, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa kuhusu uwanja huo. Katikati ni Msimamizi wa Uwanja huo, Janeth Nyoni.
Muonekano wa Jengo la  Uwanja wa Ndege  Mkoa wa Singida
Muonekano wa sehemu ya  Uwanja wa Ndege  Mkoa wa Singida.


Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge amesema kuwa Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Singida ni muhimu kutokana na kuwepo jirani na makao makuu ya nchi jijini Dododma hivyo ukarabati wake unahitajika ilikuweza kutoa huduma.

Dkt.Mahenge alitoa kauli hiyo juzi wakati alipofanya ziara uwanjani hapo kujionea hali halisi ya uwanja huo ambao hali yake hairidhishi.

Kutokana na hali hiyo Dkt. Mahenge ameagiza wasimamizi wa uwanja huo kutoka jijini Dodoma kuja mkoani Singida ilikutoa  mamaelezo na kufanya kikao cha pamoja ilikujadili  na kutambua mipaka na maeneo yote ya uwanja huo ili uanze kufanyiwa marekebisho.

Aidha Mahenge alisema kuwa mkoa wa Singida ni mkoa wa kimkakati hivyo uwanja wa ndege wa Singida ni muhimu na nia yake nikuhakikisha unatengenezwa vizuri.

Awali akitoa maelezo Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandis Paskas Muragili alisema uwanja huo wa Ndege wa Singida ni miongoni mwa viwanja  11 ambavyo vinatakiwa kufanyiwa marekebisho.

Msimamizi wa uwanja huo, Janeth Nyoni alisema uwanja huo ulianzishwa na Serikali tangu mwaka 1962 na kuwa tangu ufanyiwe tathmini ya kupanuliwa bado kazi hiyo haijaanza kufanyika.

Share To:

Post A Comment: