Kulia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali Akimkabidhi Mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu katika Skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji Madibila Bw. David Noble Mkurugenzi wa Kampuni ya  Ukandarasi ya White City International.
Bw. Shabani Sawasawa (mkulima) akizungumzia manufaa ya Mradi wa Regrow katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji ya Madibila, iliyopo katika Halmashauri ya Mbarali.

 

·      ·       MKANDARASI AKABIDHIWA KAZI

·     >  LENGO NI KUKUZA UTALII NA UCHUMI KWA KANDA YA KUSINI

 

Na: MwandishiWetu – Madibila

Ujenzi  na ukarabati wa miundombinu ya kilimo cha Umwagiliaji katika skimu ya Madibila iliyopo katika Halmashauri ya Mbarali Mkoani Mbeya, umeanza rasmi kwa mkandarasi kukabidhiwa eneo la ujenzi wa mradi na mkataba kwa  utekelezaji wa mradi huo, ambao unalengo la kusimamia ustahimilivu wa maliasili kwa ajili ya ukuaji wa utalii na shughuli mbadala  za kiuchumi  kusini mwa Tanzania.
 
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Daudi Kaale, amesema Tume hiyo inajukumu kubwa la kusimamia kilimo cha umwagiliaji nchini na kuhakikisha kwamba Skimu ya kilimo kama ya Madibila inafikia malengo yaliyokusudiwa.
 
“Uzoefu unaonesha kuwa serikali imejenga  skimu nyingi kwa gharama kubwa lakini baada ya muda hazitekelezi kazi zake au majukumu kama ilivyokusudiwa, tija na uzalishaji kupungua na hata mundombinu kuharibika.” Alisema Kaale.

Alisisitiza kuwa kuanzia sasa ni hazma ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha kuwa miundombinu yote inarejea katika hali yake ya kawaida na kufanya kazi katika malengo yaliyokusudiwa, ili kuongeza pato la Taifa, kuondoa umaskini na kuhakikisha ongezeko la ajira kwa wananchi.

Akiongea katika makabidhiano hayo msimamizi wa Mradi huo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Mkuu Ebenezer Kombe amesema,yeye kama Msimamizi Mkuu,anajukumu la kusimamia ubora, gharama halisi za ujenzi na muda wa miezi 18 ambao umepangwa kwa kazi kukamilika.

Kwa upande wake Muwakilishiwa Mkandarasi kampuni ya wazawa White City Internatinal, Bwana. David Noble amesema, wakulima watapata nafasi ya kuendelea na shughuli zao za kilimo wakati ujenzi ukiendelea, na watajitahidi kufanya  kazi kwa kiwango na wakati.

Bw.Shabani Juma Sawasawa ni mkulima katika eneo hilo,amesema kuwa, ujio  wamradi utakuwa na manufaa ya kuokoa upotevu wa maji baada ya ujenzi wa mfereji wenye urefu wa kilometa tatu kukamilika “Wakulima tutanufaika na kutunza maji pamoja na  kuyaruhusu yaende katika mto  Ruaha Mkuu kwa matumizi ya viumbe hai wengine, Maliasili na Mazingira.”Alisisitiza

Mradi huo wa REGROW ni Mradi wa usimamizi stahimilivu wa maliasili kwa ajili ya ukuaji wa utalii na shughuli mbadala  za kiuchumi kusini mwa Tanzania, Mradi ambao  unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri  ya Muungano wa Tanzania.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: