Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza na wadau pamoja na wanachi  katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika katika halmashauri ya Meru.
    Na Lucas Myovela_ ARUSHA.

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela ameitaka jamii kujenga tabia  kutunza mazingira kila siku kwa kufanya usafi huku akiwataka wadau wa mazimgira na mifumo ya serikali kushirikiane kuijengea jamii uwezo katika suala zima la mazingira.

Mongela amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika katika Halmashauri ya Meru kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ambapo alieleza kuwa ili waweze kufanikiwa katika utunzaji wa mazingira juhudi hizo zinapaswa kuwa za kila siku.

"Kwa kuwa suala la utunzaji wa mazingira na usafi ni suala ambalo lazima mtu ajengewe tabi, hivyo juhudi tunazo zifanya kwa kuwashirikisha watoto wawapo shuleni na naomba shule zote za Mkoa huu kuanza kutoe elimu hiyo ya mazingira na zitazaa matunda matunda makubwa". Ameelza Mongela.

“Tabii hii ya kutuza na kufanya usafi wa mazingira kwa sasa zitazaa matunda na kuwa mchango mkubwa kwa mazingira nchini kwetu maana wao watakuwa mabalozi wazuri kwenye jamii inayo wazunguka". Aliongeza Mongela.

Kwa upande wake Afisa mazingira kutoka baraza la taifa la uhifadhi wa mazingira(NEMC) kanda ya Kaskazini Ndg, Fransis  Nyamhanga Ameeleza  kwamba wananchi wanapaswa kutambua kuwa mazingira yao ni maisha yao hivyo watumie nishati mbadala ili kulinda na kugeuza mfumo wa ikolojia katika hali yake ya asili.

"Jamii inapaswa kupanda miti, kufanya usafi wa mazingira, kutunza vyanzo vya maji huku wakizuia ukataji wa miti hovyo na kutokutiririsha maji machafu kwenye mito kwani kila mmoja ana jukumu la kutunza mazingira ili mazigira pia yamtunze". Alieleza Fransis.
Aidha aliongeza kueleza kwamba NEMC wapotayari kufanya kazi pamoja na wadau wa mazingira ili kuhakikisha elimu ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira inawafikia watu wengi zaidi hapa Nchini na kuhakikisha nishati mbadala inasambazwa na kuweza kuokoa misitu ambayo ni rasilimali kibwa kwa taifa na jamii kwa ujumla.

“Tunajukumu la kuhakikisha mazingira ya kanda yetu na nchi nzima kwa ujumla yanakuwa mazuri kwaajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo vikute mazingira yakiwa salama na yenye faida,” aliongeza  Fransis.

Akisoma ripoti ya mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Meru afisa usafi na mazingira wa wilaya hiyo Charles Makama alisema kiwa changamoto iliyopo kwasasa ambayo inaleta madhara kwenye mfumo wa ikolojia ni pamoja na uchimbaji wa madini ya ujenzi katika eneo la ukanda wa juu ambapo ndipo kuna vyanzo vingi vya maji.
Kufuatia utumiaji wa kuni na mkaa kukithiri na kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa ikolojia ya dunia Shirika lisilo la kiserikali Dorcas Aid international liliweza kuonyesha njia mbadala ya kutumia nishati mbadala ya jiko linaloitwa mimi moto linalopika kwa muda mfupi kwa kutumia mkaa mbadala ulichakatwa kwa kutumia masalia ya mimea.

“Misitu inasaidia kilimo, mazingira na maji lakini pia inatusaidia tupata hewa safi kwahiyo sisi tumeamua kuhifadhi misitu kwakutengeneza haya majiko kama nishati mbadala kwa wakati huu kwani uharibifu unaofanyika leo unaleta athari sasa na kwa vizazi vya baadae,”Alisema Lilian Michael.
Baadhi ya wanachi wakipata ufafanuzi wa namna majiko hayo yanavyo fanya kazi.
Share To:

Post A Comment: