Na Mwandishi wetu , Dodoma


RAIS wa Jamuri ya  Muungano wa Tanzania, Samia Suluu Hassan be amempongeza, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi  kwa kuhakikisha  anashughulikia  kero za maji huku akijitahidi kujibu  maswali ya wabunge kwa weledi  hoja zinazohusu sekta hiyo bungeni.


Rais Samia ametoa kauli jana wakati akizungumza na Wanawake wa Tanzania jijini Dodoma,ambapo  amesema   Mhandisi Mahundi  amekuwa mchapakazi ambaye anapobaini kero au tatizo la maji katika eneo husika yeye kwa kushirikiana na Waziri wake, Juma Aweso  huyafikia maeneo  hayo na kushughulikia  mara moja.


“Kama mnavyosikia na kuona katika bunge kilio kikubwa ni maji maswali mengi yameelekezwa huko  Mary Mahundi, Naibu wangu anajibu mpaka  uwa namuangalia  nacheka na kimo chake na   maswali anayoyajibu  bungeni  lakini akitoka hapo ni mbio kwenye maeneo ya maji , yeye upande wake na  Wziri wake upande wake,” amesema  Rais Samia.


Amesema tangu uhuru  hadi  uongozi wa awamu ya tano , waliweza kupeleka maji kwa watanzania  asimilia 74 na kwamba  hadi sasa wanakabiliwa   uhaba wa maji kwa asimilia 26 lakini wanaendelea  kuendelea kupeleka maji  katika maeneo mbalimbali nchini kama ambavyo Waziri wa Maji anavyosema kwenye vikao vya Bunge.


Aidha Rais Samia amewahakikishia watanzania kuwa itakapofika  mwaka 2025 Serikali itakuwa imekamilisha yale yote yaliyo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi kupeleka maji  katika miji na majiji kwa asilimia 95 na vijijini asilimia 85  lengo likiwa ni kumtua mama ndoo kichwani.


Mwisho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: