Kuelekea siku ya Vipimo Duniani, Wakala wa Vipimo (WMA) wamezindua maadhimisho hayo kwa kutembelea vituo vya afya na hospitali katika eneo la Chanika na Buguruni kuhakiki mizani ambazo hutumika kwaajili ya vipimo.


Akizungumza mara baada ya kutembelea katika hospitali hizo, Meneja Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ilala Bw.Saad Haruna amesema katika uhakiki walioufanya wamegundua mizani mingi bado inausahihi unaokubarika kwa matumizi.


Aidha Bw.Haruna amesema kuwa umhumu wa vipimo katika sekta ya afya ni pamoja na matumizi ya dawa kwani ili mgonjwa apate dawa sahihi anatakiwa kupimwa uzito ili apewe dozi kulingana na uzito wake.


“Vipimo kwa maana ya mizani ni muhimu katika sekta ya afya na sisi kwa kuliona hilo na kushirikiana na uongozi wa hospitali tumekuwa tukishirikiana nao katika uhakiki wa mizani kwenye hospitali za Ilala.Lakini hii si Ilala peke yake kwasababu Wakala wa Vipimo ina ofisi nchi nzima hivyo maadhimisho haya yamefanyika nchi zima katika mikoa na wilaya zote nchini”. Amesema Bw.Haruna.


Kwa upande wake Muuguzi wa Kituo cha afya mama na mtoto Chanika Bi.Barry Fundi amewashukuru Wakala wa Vipimo kufika na kuhakiki mizani katika kituo hicho kwani kupitia hivyo kuna wapa mwangaza kuwa huduma wanazozitoa ni sahihi hata kwa vipimo vya dawa wanavyovitua kwa watoto kulingana na uzito kwa maana watoto wengi wanapewa matibabukulingana na uzito wao.


Nae fundi sanifu vifaa tiba katika kituo cha afya Buguruni Bw.Gidion Maganga amesema uhakiki wa mizani kwenye vipimo kwa maana inaongeza kitu katika matibabu yake ambapo itamsaidia kufahamu ni matumizi gani ya dawa anaweza kutumia na zisimletee madhara.


“Kuna wale ambao wanadharau mizani hizi ni hatari kwao kwasababu utakuja kupata dawa ambazo hazijaendana na uzito wao kitu ambacho kitaweza kukuletea madhara katika afya zao kwani hautakua unafahamu ni dozi gani unatakiwa kutumia”. Amesema Bw.Maganga.


Maadhimisho haya hufanyika Mei 20 kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA”.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: