Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga 

Na Kadam Malunde
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeendesha semina kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.

Semina hiyo ya Siku tatu iliyoanza leo Jumatatu Mei 10,2021 katika ukumbi wa Nashera Hoteli mkoani Morogoro imekutanisha pamoja waandishi wa habari mtandaoni kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar. 

Katika Semina hiyo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) wameiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, iondoe sheria  zote kandamizi zinazoathiri uhuru wa vyombo vya habari.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga ametoa ombi la kufutwa kwa sheria zinazolamikiwa, wakati akizungumzia agizo la Rais Samia, alilolitoa hivi karibuni la kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa kutokana na sababu mbalimbali.

Amesema agizo la Rais Samia sio suluhu ya changamoto ya vyombo vya habari kufungiwa na kuminywa visifanye kazi zake kwa uhuru, bali inatakiwa sheria zibadilishwe ili uhuru wa vyombo vya habari uenziwe na viongozi watakaofuata.

"Rais Samia akiapisha Makatibu Wakuu, aliongelea kidogo suala la uhuru wa habari na aliagiza vyombo vifunguliwe. Hili lina mjadala sababu wengine tulisikia ametamka vyombo vya habari lakini wasaidizi wake wamesema agizo lilihusu vyombo  ya habari vya mtandaoni. Kwa sababu ofisi yake haijatoa kauli juu ya tarifa ya wasaidizi wake hao, agizo la kufunguliwa mtandaoni bila shaka hilo ndiyo sahihi," amesema Mukajanga.

"Tunadhani bila kushughulikia sheria zinazoongoza, zinazosimamia na kudhibiti kazi zetu, tatizo halitaweza kuondoka. Kwa nia njema hiyo, anaweza akaamua kama hivyo mfungulieni flani, lakini kama sheria ipo maana yake kesho anaweza pata tatizo mtu mwingine au yuleyule aliyefunguliwa akapata tatizo kutokana na sheria zile zile," amesema Mukajanga.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF) Deodatus Balile amesema, mchakato wa mabadiliko ya sheria za mtandaoni umeanza kufanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuwaomba wadau kujitokeza kutoa maoni

Amesema kauli ya Rais Samia haikusema vyombo vya habari vya mtandaoni, "alisema vyombo vya habari vilivyofungiwa, vifunguliwe" na akagusia suala la kanuni ziwe wazi hivyo mkanganyiko ulikuja kwa watendaji wa Rais Samia wamekuwa waking'ang'ana ni vya mtandaoni pekee jambo ambalo linaendeleza mjadala wa agizo hilo la Rais.

"Bila kushughulikia sheria,zinazodhibiti kazi zetu changamoto hazitaondoka. Mchakato wa mabadiliko ya sheria tayari umeanza. Vyombo vya habari mtandaoni tunaomba tushiriki kwani TCRA imeanza, tukatoea mawazo yetu," amesema Balile.

"Hivi sasa kazi zenu zina walaji wengi, mnafikia watu wengi sana hivyo ni muhimu Online Journalism iende vizuri kwa kusimamiwa vizuri, na wanaosimamia online wanatakiwa kuwa watu wazuri. Sisi waandishi wa habari, tuonyeshe weledi kidogo katika kuhabarisha umma",ameongeza.

Naye Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo amesema ni vyema Sheria na kanuni kandamizi katika tasnia ya habari ziondoshwe ili uhuru wa kujieleza uwepo

Kwa upande wake Mratibu wa THDRC, Onesmo Ole Ngurumwa alisema, semina hiyo ina lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mtandaoni ambao ni eneo linalokuwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni na kutokana na uwepo wa sheria mbalimbali kandamizi kwa eneo la usimamizi wa vyombo vya habari, wamefungua kesi mahakamani ya kuzipinga.

Amesema mwisho wa mafunzo hayo ya siku tatu, yatawafanya waandishi wa habari wa mitandoni kuwa na uelewa mpana wa masuala mbalimbali ili waweze kutimiza majukumu yao kwa weledi.

"Lengo la semina hii ni kuwajengea uwezo ili wafanye kazi vizuri katika kuhabarisha watanzania kwa sababu watu wengi wamehamia mtandaoni. Kundi hili la waandishi wa habari mtandaoni ni muhimu kulisaidia ambapo mpaka sasa vyombo vya habari mtandaoni vilivyosajiliwa ni zaidi ya 400 hivyo kuna wimbi la ukuaji",amesema.

"Siyo kila mtu anayeendesha mtandao ni mwandishi wa habari. Siyo kila mtumiaji wa Youtube Channel ni mwandishi wa habari,baadhi yao hawana taaluma ya habari, lakini siyo kila mtu mwenye channel anapaswa kusajili TCRA. Vyombo vya habari vya mtandaoni zimetungiwa sheria na kanuni za kujiendesha. Tuendelee kupigia kelele kanuni hizi ili tupate kanuni rafiki”,ameongeza Ole Ngurumwa.

 TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF) Deodatus Balile akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.

Mratibu wa THDRC, Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.

Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.

Mwandishi wa Habari Salma Said kutoka Zanzibar akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini

Share To:

msumbanews

Post A Comment: