Meneja Mwandamizi wa mradi kutoka Shirika la Farm Africa, Tumaini Elibariki (wa pili kushoto) akimpa maelezo  ya kilimo chenye tija cha zao la Alizeti Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (wa pili kulia) wakati alipotembelea shamba darasa la zao hilo katika Maadhimisho ya Mkulima Shambani yaliyofanyika Kijiji cha Mnang'ana Kata ya Sepuka jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi na kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ally Mwanga.



Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo akihutubia kwenye maadhimisho hayo.



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akizungumza kwenye maadhimisho hayo.



Meneja Mwandamizi wa mradi kutoka Shirika la Farm Africa, Tumaini Elibariki, akihutubia kwenye maadhimisho hayo.





Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Farm Africa, Mratibu Mwandamizi wa shirika hilo, William Mwakyami, akizungumza wakati akitoa salamu za Mkurugenzi huyo kwenye maadhimisho hayo.



Mjasiriamali Juma Mwangi kutoka Kijiji cha Mtinko akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo alipokuwa akitembelea mabanda.
Meneja wa Wakulima wa Kampuni ya Pyxus, Edwin Shio   akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo alipokuwa akitembelea mabanda.


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akipata maelezo alipotembelea banda la Benki ya NMB.

Meneja wa Mbegu kutoka Kampuni ya Daudi Yamagaji Bytrade Tanzania Ltd., akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Afisa Masoko kutoka Kampuni ya Zamsee, Juliana Massao akizungumza katika maadhimisho hayo.
Mjasiriamali Amina Daffi  kutoka Kijiji cha Mtinko, akizungumza katika maadhimisho hayo

Mdau wa Kilimo, Ahmed Kaburu, akizungumza katika maadhimisho hayo



Muonekano wa shamba darasa la Alizeti kwenye maadhimisho hayo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga, akizungumza katika maadhimisho hayo.

Vyeti vikitolewa kwa washindi.

Mmoja wa washindi na wenzake wakifurahi wakiwa wamemba mbuzi waliozawadiwa.
Diwani wa Kata ya Sepuka Halima  Nyimba akizungumza  kwenye maadhimisho hayo.



Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo amesema Mkoa wa Singida umejipanga kukabiliana na uhaba wa mafuta ya kula na kuwa ukiamua kujidhatiti kwa dhati katika kilimo cha alizeti unaweza kuilisha nchi yetu.

Mpogolo ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo jana katika maadhimisho ya siku ya mkulima shambani yalifanyika Kijiji cha Mnang'ana Kata ya Sepuka wilayani humo na kuandaliwa na Shirika la Farm Africa kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na usawa wa kijinsia na wanawake (UN Women) kwa kushirikiana na Koica. 

" Singida tuna viwanda vikubwa na vidogo zaidi 175 ambavyo vinauwezo wa kuhitaji tani 350, 000 ambayo inafafana na upungufu wa alizeti nchini wa tani 360,000  hivyo tukikomaa na kupambana tunaweza kuilisha nchi na kupata bilioni 188." alisema Mpogolo.

 Mpogolo alisema tukiichukua asilimia 40 tuliyo nayo sasa na kuijumlisha na bilioni 100 tunakwenda karibia bilioni 300 ambazo tunaweza kuzitafuta kwenye kilimo cha alizeti hivyo kwanini wakaangaike kutafuta mbao kwenye hifadhi na kuchoma mkaa na kujikuta wakikamatwa na askari.

Aidha Mpogolo alisema kwa takwimu zilizopo uhitaji wa mafuta ya alizeti hapa nchini ukilinganisha na idadi yetu zaidi ya milioni 60  ni kati ya tani 400,000 hadi 570,000 na kuwa uzalishaji uliopo ni asilimia 40 huku asilimia 60 tukiagiza kutoka nje ambayo ni wastani wa tani 360,000 kwa thamani ya dola karibia milioni 80.

Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya mkulima wa wilaya hiyo alisema kilimo cha alizeti mkoani Singida hususani wilayani Ikungi ni adhima ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuona zao hilo linahimarika.

Alisema wilaya hiyo itafanya kila liwezekanalo na kuona kilimo hicho kina wapeleka mbele.

Aidha Kijazi akizungumzia mradi huo unaofadhiliwa na UN Women, Koica chini ya wadau wengine wakiwepo Farm Africa kuanzia mwaka jana,  mradi huo wa miaka mitatu utagharimu zaidi ya bilioni 5.2 na kuwa umegawanyika katika aina kuu tatu, kilimo cha alizeti ambacho kinaongozwa na Farm Africa, Kilimo cha mbogamboga kinachoongozwa na TAHA na Mradi wa kuwawezesha wanawake kijinsia.

Alisema kwa mwaka huu wa mradi takribani dola 900,000 zimeruhusiwa na Koica na zinaendelea kufanya kazi katika maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Meneja Mwandamizi wa mradi kutoka Shirika la Farm Africa, Tumaini Elibariki  alisema shirika hio kwa kushirikana na UN Women lina wawezesha wakulima wadogo hususani wanawake na vijana wa Wilaya ya Ikungi katika Kilimo cha Alizeti. 

Alisema katika kipindi cha kuanzia mwaka huu kati ya January 21 na January  20, 2022 Farm Africa kwakushirikiana na UN women chini ya ufadhili wa KOICA imepanga kutumia takribani Sh. Milioni 309 kwa ajili ya mafunzo ya wakulima 350 kutoka katika kata 3 za Sepuka, Irisya na Dung’unyi na ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao katika Kijiji  cha Mnang’ana. 

Aidha Elibariki alisema wakulima katika wilaya hiyo wanayo nafasi nzuri ya kuongeza uzalishaji na kuchukua fursa ya kufunga mkataba na wanunuzi ili kuhakikishiwa wanapata mbegu bora na zenye tija kama walivyoona kupitia shamba darasa kwenye maadhimisho hayo. 

Elibariki alisema kuwa mradi huo kwa kipindi cha miezi mitano umewafikia wakulima zaidi ya 300  sawa na asilimia 65 ya wanawake kati yao vijana ni asilimia 30 kutoka katika Kata za Sepuka, Irisya na Dungunyi. 

Aliwataja wadau wengine walioshiriki maadhimisho hayo kutoka Sekta Binafsi kuwa ni washirika wa mradi kutoka mashirika ya wasindikaji, wakubwa na wadogo, TCCIA, Pyxus, Bytrate-Advanta, Taasisi za Fedha (TADB, NMB, TPB, NBC, CRDB, PASI) kutoka maeneo  mbalimbali ndani na nje ya wilaya  ya Ikungi ambao kimsingi ni wa muhimu katika kutoa huduma wezeshi ndani ya Mnyororo wa thamani wa zao la Alizeti wilayani Ikungi na Tanzania kwa ujumla. 

Share To:

Post A Comment: