NA Lucas Myovela, ARUSHA.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala bora Mhe: Mohamed Mchengerwa kesho anatarajiwa kufungua mkutano wa chama cha makatibu mahusi Tanzania {TAPSEA} ambao umekutanisha  makatibu 2900  kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura Songambele Maganga alisema kuwa mpaka sasa makatibu mahususi 2900 wameshawasili katika mkutano huo ambao utakuwa na agenda mbalimbali ya masuala yanayowahusu na wanatarajia kuwa na Mhe:Mchengerwa katika ufunguzi wa kikao cha hapo kesho.

Alisema kuwa mkutano wao utajadili kwa kina mapungufu na mapendekezo yaliyopo katika fani hiyo kama ambavyo walivyofanya mwaka 2017 ambapo waliweza kushinikiza kuwepo kwa elimu ya juu{Degree} katika fani hiyo jambo ambalo lilifanikiwa na sasa wamepata fursa hiyo.

“ Kupitia mkutano huu tutajaribu kuongea na serikali kuhusiana na changamoto tulizonazo pamoja na mapungufu yaliyopo katika fani yetu pamoja na kupean mikakati ya kuwa waadilifu na kuwa watumishi wenye maadili pamoja na kuchapa kazi kwa weledi,” Alisema Bi Mganga.

Alifafanua kuwa kwasasa wana soko la ushindani wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo wakiweka makatibu mahususi tu maofisini bila kuwakumbusha majukumu yao katika kuzifanya ofisi zao kufanya vizuri hawawezi kuwa wapya ndio mana wanakutana.

Kwa upande wakekatibu wa chama hicho Aneth Charles Mapima alieleza kuwa kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu ni “kuwa mbunifu mahiri, zingatia weledi katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi Tanzania” na kuendea kusema kuwa makatibu mahususi ni ni taswira ya ofisi kwani wamebeba majukumu makubwa .

“Tumeamua kuweka hii mikutano kila mwaka ili kuleta amsha amsha kwa makatibu katika kutenda kazi katika ofisi mbalimbali kwani wanahitaji kupata ujuzi mpya na maarifa mapya kila mwaka ili kuweza kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia katika nchi yetu,”alisema  Bi Mapima.

Hata hivyo mpaka mkutano huo utafnyika kwa sili mbili ambapo tarehe 21.5.2021 utawahusisha makatibu mahususi wote na tarehe 22 utawahusisha makatibu ambao ni wanachama wa chama hicho ambao wapo 2500.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: