Kaimu Mkuu wa Utawala wa JKT Kanali Hassan Mabena,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za JKT zilipo Chamwino Dodoma leo Mei 22,2021  kuhusu kuwataarifu vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2021 wametakiwa kuhudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria .


Na.Alex Sonna,Dodoma 

Jeshi la kujenga taifa JKT limewataka wanafunzi waliohitimu kidato cha sita kwa shule za Tanzania bara kwa mwaka 2021 kuhudhuria katika mafunzo ya JKT katika  makambi mbalimbali ya jeshi hapa nchini kuanzia juni 1 hadi 10 mwaka 2021.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la kujenga taifa Brigedia Jenerali Rajabu Mabele, Kaimu Mkuu wa utawala JKT Kanali Hassan Mabena amesema sambamba na wito huo JKT limewapangia wakambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo.

“Jeshi la kujenga taifa JKT linawaita vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2021, kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria na wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 1 hadi 10 june 2021” amesema Kanali Mabena.

Amesema vijana wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT Rwamkoma, Mara, JKT Msange Tabora, JKT Ruvu Pwani, JKT Mpwapwa na Makutopora Dodoma, JKT Mafinga Iringa, JKT Mlale Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba Tanga, JKT Makuyuni Arusha, JKT Burombera, JKT Kanembwa na JKT Mtabila Kigoma, JKT Itaka Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa Rukwa, JKT Nachingwea Lindi, JKT Kibiti Pwani, na JKT Oljoro Arusha.

Aidha Kanali Mabena amesema kwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho waripoti katika kambi ya JKT Ruvu Pwani kwani ni kambi yenye miondombinu kwa watu wenye ulemavu na wanauwezo wa kuhudumia watu kama hao.

Aidha JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa kama bukta ya dark blue yenye mpira kiunoni na yenye mifuko mirefu na yenye zipu, T shert ya rangi ya kijani, raba za michezo zenye rangi ya kijani na blue, shuka mbili za kulalia zenye rangi la blue bahari.

Vifaa vingine ni Soksi ndefu za rangi nyeusi, nguo za kujikinga na baridi kwa waliopangiwa kwenye mikoa yenye baridi, track suti ya rangi ya kijani au blue, nauli ya kwenda na kurudi nyumbani, Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana wote kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za Maisha na utayari wa kulijenga taifa na kulitumikia taifa.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: