Na Angela Msimbira TAMISEMI


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Gerald Mweli amewataka  Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi kuhakikisha wanaanzisha mtandao ambao watatutumia kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa Miradi ya maendeleo.


Ameyasema hayo leo wakati  akifungua Mkutano wa siku tatu wa Umoja wa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA), uliofanyika Jijini Dodoma wenye kauli mbiu ya mipango  na bajeti inayozingatia  huduma endelevu za jamii.


Amesema kwa sasa kumekuwa na changamoto  kubwa ya kusuasua kwa utekelezaji wa miradi katika baadhi ya halmashauri pamoja  na Serikali  kutoa  fedha kwa pamoja na kwa wakati


“Kuna baadhi ya halmashauri zimepelekewa fedha za ujenzi wa mabweni shilingi Mil 80, kuna wengine wamemaliza na kuweka na vitanda lakini wengine bado. Hata pale serikali inapotoa fedha za ujenzi wa madarasa halmashauri mmoja inaweza kuona Sh milioni 20 zilizotolewa hazitoshi lakini kuna wengine kwa kiasi hicho hicho wanamaliza na madawati ndani, sasa kutumia mkianzisha mtandao huo itakuwa rahisi kushirikisha wenzako uzoefu huo ili nao waweze kamilishe mradi huo” amesema Mweli.


Ameendelea kufafanua kuwa uanzishwaji wa mtandao wa kujifunzia kutasaidia kujifunza changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika Halmashauri  hasa katika suala zima la utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.


Mweli pia amewataka watendaji hao kutumia  mtandao  huo kubadilishana uzoefu kuhusu njia mbora ya utekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yao kwa kutumia mfumo wa force akaunti na kwa kutumia mkandarasi.


 Amesema kuwa Serikali kwa sasa inaanza kutoa fedha kwa ajili ya halmashauri mpya ambazo hazina makao makuu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi, jambo ambalo nataka niwasisitizie ni kwamba hili si jipya Tanzania kuna halmashauri zimejenga ofisi kwa kutumia fedha za ndani hivyo  badilishaneni uzoefu wa kati ya halmashauri mmoja na nyingine.


“ Mfano kwenye sekta ya elimu tunamatatizo kwenye ujenzi wa mabweni, kuna halmashauri zimemaliza ujenzi na zingine bado  wakati ni maeneo yanafanana, labda kuna sababu basi tutumie mtandao huo kushirikishana maana siku  ya mwisho miradi hii ikamilike.”amesisitiza mweli


Aidha  Mweli amewataka kusimamia vizuri rasimali watu katika maeneo yao kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu, miongozo na nyaraka zinazosimamia utumishi wa umma


“ Jambo hili limekuwa likituchukulia muda mwingi sana, pale Ofisi ya Rais Tamisemi  kwa kusikiliza rufaa kwa baadhi ya watumishi ambao kwa namna moja au nyingine wanaona hajatendewa haki lakini pia tumekuwa tukipata malalamiko mengi kwa watumishi wapya wa kada ya afya pindi wanaporipoti kazini kwa mara ya kwanza kumekuwa na ucheleweshaji sana wa kuwapa fedha za kujikimu.”

Share To:

msumbanews

Post A Comment: