Teddy Kilanga


ARUSHA


SERIKALI  imekitaka Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS )kuachakujihusisha na masuala ya kisiasa na uanaharakati badala yake kijikite zaidi kusaidia jamii katika nyanja za kisheria.


Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa TLS uliofanyika jijini Arusha,Naibu katibu Mkuu wa wizara ya Sheria na Katiba,Amon Mpanju,alisema 

pamoja na Mambo mengine Mkutano huo utamchangua irais mpya kuchukua nafasi ya aliyemaliza muda wake huku akikitaka chama hicho kuendeleza misingi ya sheria.


Mpanju ambaye kitaaluma ni wakili,alisema kuwa kumekuwepo na Baadhi ya

Viongozi wanaochaguliwa na TLS kuendesha harakati za kisiasa na

kusahau majukumu yao Jambo hiloolisifanyike na chama hicho kijikite kutetea haki za wananchi.


Amewataka  wanachama wa TLS wanaofikia 10,000 hapa nchini kuzingatia

maadili ya taaluma yao ,kuwa na mienendo mizuri Katika kufuata utawala

wa kisheria.


"Kuna mawakili wamekuwa na tabia ya kuchukua fedha za wateja wao na

kushindwa kuwawakilisha vizuri na wengine kutelekeza mashauri

yao,Jambo Hilo si jema Sana na wanapaswa kubadilika na kuzingatia

miiko ya kazi yao"alisema.


Katika hatua nyingine Mpanju ameonya mawakili wa serikali wapatao 1703

ambao Baadhi yao wanajihusisha  na uwakili wa kujitegemea nje na

utaratibu, kuacha Mara moja na kuwataka wenye tabia hiyo kuchagua moja

Kati ya uwakili wa serikali ama kujitegemea.


Ameitaka TLS kujikita zaidi kwenye misingi ya kuendeleza tasinia ya

kisheria na Viongozi wanaochaguliwa wajitafakari na kuja na mbinu mpya

ya kuwatetea wananchi.


Awali Rais wa TLS  anayemaliza muda wake, Dkt Rugemereza

Nshalla,amesema kuwa TLS imekuwa na Changamoto mbalimbali hali

iliyofanya kushindwa kufikia malengo yake Katika kipindi cha miaka

miwili.


Alizitaja Baadhi ya Changamoto hizo kuwa ni pamoja na mabadiliko ya

kisheria hapa nchini,Ugonjwa wa Corona ,Baadhi ya wanachama

kubambikiwa kesi zikiwemo za utakatishaji fedha,wanachama kutishwa na

wengine kufutiwa leseni ,kuhuisha leseni na kutakiwa kujisajili Kodi

ya ongezeko la thamani (VAT).


Hata hivyo dkt Nshalla alisisitiza kuwa TLS itaendelea kupigania na

kutetea haki za wananchi pamoja na wanachama wake ikiwemo wanachama

waliofungiwa leseni zao.


Chama hicho Cha wanasheria Tanganyika kinatarajia kufanya uchaguzi

hapo kesho(leo) kumpata rais mpya baada ya Dkt Nshalla kumaliza muda

wake,ambapo wagombea watano watachuana vikali kuwania nafasi hiyo

ambao ni Albert Msando,Dkt Edward Hosea,Flaviana Charles,Fransis

Stolla na Shehzad Walli.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: