Na Esther  Macha, Mbeya


MKURUGENZI wa  shule ya  mchepuo wa kiingereza ya Holyland iliyopo katika Mji wa Makongolosi Wilayani chunya Mkoani Mbeya , Lawena Nsonda (Maarufu kwa jina la baba mzazi )amesema kuwa Tanzania imeandika historia mpya ya kupata Rais Mwanamke na kuona kuwa tayari  Rais Samia Suluhu ameanza kuona madhaifu na kuwa mkali na kuchukua hatua .


Amesema kuwa  wale waliokuwa wakibeza na kusema wamepata mama ambaye atakuwa anambembeleza wameona kuwa akina mama wakiwa kazini wanakuwa si watu wa  mchezo mchezo wanakuwa ni wakali kweli kweli si watu wa kuwadharau kama ambavyo watu walibeza kwa mama Samia.


Nsonda amesema hayo jana wakati akizungumza na Msumba News Blog ofisini kwake kuhusiana na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya watu kuwa wanawake hawawezi kuongoza  kuliko wanaume  .


Mkurugenzi huyo alisema kuwa  watanzania  wanatakiwa kushirikiana kwa pamoja na kumwombea Rais na kumpa ushirikiano ili mambo yaweze kuwa mazuri zaidi na zaidi .


“Tumeona Mh. Rais Samia  tayari ameanza kufanya kazi vizuri na  tayari ameanza kuangalia kwenye udhaifu na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika  tumpe ushirikiano ndugu zangu Rais wetu ni kiongozi mzuri tufanye nae kazi anaweza”alisema Nsonda.


Akizungumzia kuhusu kubadilika kwa watendaji serikalini katika kumuenzi Hayati Magufuli ni kufanya yale ambayo alikuwa akiyataka kufanya ambayo ni  uzalendo, uchapaji kazi kama ilivyonekana maeneo mengine walivyofanya kuombeleza kwa kuchonga majeneza kwa kuandika jina la Magufuli kwamba wanaenda kuzika wengine walishindwa kula chakula kwa siku nzima kwamba jinsi Magufuli ambavyo alikuwa akifanya kazi Nchi zingine  Marais waliiga mfano wa utendaji kazi wa Hayati Magufuli .


“Tulipata Rais ambaye aliweza kuiweka Tanzania katika mstari  ulio mzuri alikuwa na upekee wake ambao ulifannya Nchi zingine kutoa mfano wa utendaji kazi wake “alisema Nsonda.


Hata hivyo Mkurugenzi huyo alisema kwamba Rais Samia katika kumuezi hayati Magufuli kwa kile alichokuwa akifanya  alikuwa Rais mkali alikuwa hapendi mchezo ,alipenda watoto hivyo Mh Samia aweze kufanya kazi kwa bidii kuonyesha kile ambacho hayati magufuli alikuwa akifanya.


“Nilifurahi jana wakati akipokea ripoti ya (CAG )alimtolea mfano  Waziri Jaffo kuwa hayati Magufuli aliwahi kumuonya  kutokana na uzembe unaofanyika na mimi nakuonya leo kwa hiyo utaona kwamba Rais Samia nae ameanza kuchukua yale aliyokuwa akifanya hayati Magufuli “alisema Nsonda( baba mzazi) .


Akizungumzia kuhusu sekta ya madini Mkurugenzi huyo alisema kuwa mara ya kwanza katika sekta ya madini  watu walikuwa hawajui masoko ya dhahabu  na serikali ilikuwa inapoteza mabilioni ya fedha kwa kutokuwa na masoko ya dhahabu na hayati Magufuli alianzisha masko ya dhahabu nchi nzima .


Aidha Nsonda alimwomba Rais Samia kuimarisha ulinzi zaidi kama ilivyo merereni na mawaziri waweze kuwa na ustaarabu na nchi yao kama ambavyo alivyofanya  hayati Magufuli .


Mwisho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: