Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.John Pima akizungumza katika kikao Cha siku moja Cha kujadili namna ya kukuza utalii katika Jiji la Arusha.

Meya wa Jiji la.Arusha Maximillan Irange kikao Cha siku moja Cha kujadili namna ya kukuza utalii katika Jiji la Arusha

Mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo akichangia mada katika kikao Cha siku moja Cha kujadili namna ya kukuza utalii katika Jiji la Arusha:Mgeni anapotembelea sehemu Jambo la kwanza anatakiwa kuhakikishiwa ni Usalama wake.

Wadau mbalimbali wakiwemo Wadau wa Utalii wkaifuatilia mjadala katika kikao kilichofanyika New Arusha Hotel Jijini Arusha

Baadhi ya wadau wa maendeleo na wadau wa utalii wakiwa katika mkutano kikao Cha kujadili namna ya kukuza utalii katika Jiji la Arusha

Baadhi ya wadau wa maendeleo na wadau wa utalii wakiwa katika mkutano kikao Cha kujadili namna ya kukuza utalii katika Jiji la Arusha,pamoja na kuangalia Changamoto mbalimbali na namna ya kuzitatua




Na.Vero Ignatus,Arusha

Katika kutekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan chini ya mkurugenzi wake Dkt.John Pima,amewasilisha mkakati wake mbele ya wadau mbalimbali wakiwemo wadau wa Utalii Jijini Arusha, lengo likiwa nikukaribisha uwekezaji mkubwa katika Jiji hilo ili liwe Kitovu cha utalii kwa vitendo.

Akizungumza katika kikao cha siku moja kilichofanyika New Arusha Hotel Mkurugenzi Pima alisema :yapo mambo mengi ambayo wakishirikiana serikali na wadau kutokana na Jiografia iliyopo, wanaweza kufanya vizuri zaidi ,kwani wanataka kutumia fursa hiyo kuboresha mazingira,na kuangalia namna gani wanaweza kurudhisha hadhi na heshima ya Jiji la Arusha

‘’Tunawakaribisha ninyi wadau mje na maandiko mazuri ,ambayo yatasababisha haya mambo yatokee,sisi tunao wataalam lakini ninyi pia mnao wataalam,njooni tukae Pamoja tuyajenge ili kuhakikisha Arusha inakuwa mpya na yenye maendeleo zaidi’’Alisema Pima

Aidha Pima amesema Jiji hilo limefungua milango kwa wawekezaji kwaajili ya kuleta maendeleo na kuhakikisha kuwa wageni wanaongezeka kwa wingi na kukuza uchumi wa Jiji hilo na kuongeza pato la Taifa kupitia sekta hiyo ya Utalii.

Akizungumza Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Maximillan Irange alisisitiza kuwa muda wa michakato katika umekwisha ,hivyo sasa ni muda wa kazi na vitendo zaidi,hivyo lazima maisha yaendelee,kwani katika jiji la Arusha kuna fursa nyingi sana za uwekezaji pamoja na utalii,muda mwingi unapopotezwa huwa unawakatisha tamaa wawekezaji.

Irange amewahakikishia wadau hao kuwa watapanga kwa pamoja namna ya kufanya uwekezaji wa kina katika bonde la mto Themi,bonde la mto Naura ,mlima Suye na kwa mrombo kweye nyama choma na sehemu mbalimbali za vivutio katika jiji la Arusha .

Kwa upande wake mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo alichangia kwa kuanza na swali kwamba :Ni lazima kila mmoja ajiulize!ni jambo gani lililochangia kuharibu utalii katika jiji la Arusha?Aidha alianisha kwa kusema kuwa ili mtalii aweze kutembelea sehemu lazima ahakikishiwe usalama wake,usafi wa mazingira halisi,huku akianisha hali ya kisiasa imechangia utalii kushuka

Chambulo aliweza kutoa ushauri kwa viongozi wa Jiji la Arusha kwamba ikiwezekana waweze kutengeneza City Park kwaajili ya wageni, pamoja na watu mbalimbali na familia zao kufanya utalii wa kutembea katika maeneo ya vivutio katika Jiji,huku akiwataka wadau kuondokana na dhana potofu kwamba city park siku zote ni mali ya wazungu

Aidha Chambulo kwa niaba ya wadau wa utalii aliweza kuwasilisha ombi kwa viongozi la kukutana na wabunge wote Tanzania Bara,na visiwani ambapo wanahitaji kuzungumza nao kwani wao ndio wanaotunga sheria,na kuona namna ambayo wanaweza kuiuza Arusha na Tanzania hususani kwenye Utalii.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: