Jane Edward,Msumba News,Arusha

Waziri wa mawasiliano ,Teknolojia na habari Dokta Faustine Ndugulile ameitaka  mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)  kudhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria matapeli  wa mitandao ya simu  ambao wamekuwa wakiwaibia wananchi.


Ameyasema hayo leo akiwa kwenye ziara yake ya kutembelea Taasisi mbalimbali  zilizopo chini ya wizara yake katika kujionea utendaji kazi na changamoto mbalimbali .


Dokta Ndugulile amesema kuwa,kumekuwepo na wizi mbalimbali unaofanywa katika mitandao ya kijamii ambao umekuwa ukisababisha adha kubwa kwa wananchi,hivyo ni jukumu la kuhakikisha wanawachukulia hatua Kali za kisheria wanaohusika na utapeli huo.


Amesema kuwa,Mamlaka hiyo ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha wananchi hawatapeliwi kupitia mitandao mbalimbali badala yake wadhibiti ikiwemo kuwachukulia hatua za kisheria ili uhalifu huo uweze kukoma.


Aidha alitaka kutolewa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya Tehama kwani swala la elimu bado ni changamoto kubwa Sana kwa wananchi ,hivyo ni vizuri watoe elimu inayoenda sambamba na upatikanaji wa vifaa.


"Tunawaomba sana muendelee kutoa elimu kila  siku juu ya mitandao ya kijamii ,na elimu ya haki na wajibu na hatua za kuchukua pia ili wananchi waweze kuzitambua haki zao za msingi".amesema.


Aidha amewataka wananchi kutambua kuwa  gharama za kupiga simu nje ya nchi zimepungua Sana Sasa hivi ,hivyo wananchi wasiogope kwani serikali hawana lengo la kuzuia matumizi ya kwenye mitandao bali kuboresha huduma zaidi.


Naye Meneja wa TCRA Kanda ya kaskazini ,Imelda Salum  amesema kuwa ,wametoa elimu kwa wananchi  juu ya kuweza kutambua wajibu na haki zao pamoja na matumizi salama ya mitandao,makosa ya mitandao na namna ya kuwasilisha  changamoto zao pindi wanapokutana nazo.


Amesema kuwa,wanafanya ufuatiliaji wa masafa kwa watoa huduma na upimaji wa masafa ,sambamba na kutoa elimu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano kama vile  radio, television na watoa huduma za mitandaoni .


Share To:

msumbanews

Post A Comment: