Mhandisi, Meneja Umwagiliaji wa  mradi shirikishi wa kilimo cha Umwagiliaji Mwisa Wilayani Karagwe Bw. Adelialidy Mwesigwe akizungumza baada ya kupokea baadhi ya vifaa vinavyotumika katika ukarabati kwenye skimu hiyo.


Picha Ikionesha sehemu ya Barabara katika Skimu hiyo kabla ya kuanza ukarabati.

Mwendesha Mitambo Bw. Kuchada Faustine, akishindilia tuta kwa tumia mashine aina ya (Hand Roller Compactor) wakati wa ukarabati katika skimu

 Kulia Meneja Mradi Shirikishi Mhandisi Adelialidy Mwesingwe akihakiki baadhi ya vifaa vitakavyotumika katika ukarabati kwenye Skimu ya Mwisa Wilayani Karagwe, kushoto ni Mpima Ardhi Bw.Ombeni Justo Ikola.

Na; MwandishiWetu, Karagwe–Kagera

Ukarabati wa Miundombinu ya Kilimo cha umwagiliaji Wilayani Karagwe Mkoani Kagera Umeanza Rasmi, kwa ujenzi wa Barabara katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Mwisa pamoja na mifereji ya kupitisha maji kuelekea mashambani.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa vya ujenzi Mhandisi wa Umwagiliaji, ambaye pia ni Meneja Maradi huo shirikikishi Bw.Adelialidy Mwesigwe, Amesema amepokea baadhi ya vifaa ambavyo vitaweza kutumika katika ujenzi pamoja na kusakafia mfereji wenye urefu wa mita mia saba hamsini (750).

Ambapo mpaka sasa mtaro wenye urefu wa mita miatano na mbili (502) umeshachimbwa na barabara yenye urefu wa mita mia saba na sitini (760) inayokwenda sambamba na mtaro huo imekwishaandaliwa.

“Tutajenga vikinga maji tisa, (9)  kwenye awamu hii kutokana na kwamba skimu hii inaukubwa wa eneo la Hekta miatatu (300) ambalo linalimwa zao la mpunga na mazao mchanganyiko.” Alisema Mwesigwa.

Aliendelea kusema kuwa eneo ambalo lipo nje kidogo wakulima wanalima bustani za mboga mboga, na Skimu ina idadi ya wakulima mia moja na sabini na tano (175).


Miradi hii shirikishi ya maendeleo ya serikali ya awamu ya tano katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji inashirikisha wananchi wakazi waeneo husika katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu hiyo.





Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: