Tuesday, 2 March 2021

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO ASEMA MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO CHALINZE ITAIMARISHWA

 

NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE.

 NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (ICT) - Mhandisi. Andrea Mathew Kundo amemwagiza Mkuu wa Kanda wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Kanda ya Mashariki kushughulikia haraka maombi ya Halmashauri ya Chalinze ya kuimarisha MIundombinu ya mawasiliano.
 Hatua hiyo ni pamoja na kupatiwa kibali cha Masafa ya radio (radio frequency) na Televisheni ambayo yalikwama kwa muda. Aidha mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameeleza ,Halmashauri ya Chalinze,imepokea vifaa kwa ajili ya kupimia Ardhi.

 Vifaa hivyo vinasaidia kurahisisha Upimaji ambapo vitawezesha kwa siku kupimwa kwa viwanja hadi 200 toka utaratibu wa kawaida wa viwanja 5.

No comments:

Post a Comment