Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh. Maxmilillan Matle Iranqhe ameahidi kufanya ukarabati  wa miundombinu ya Shule ya Msingi ya Kimandolu itakayogharimu Milioni Kumi {10,000,000} lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule hiyo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa karo la kunawia mikono kwa ajili ya kuboresha Afya za Wanafunzi Mstahiki Meya amesema ukarabati huo mkubwa katika shule hiyo utafanyika haraka kutokana na mwelekeo wa Serikali wa Awamu ya Tano ya kuhakikisha kwamba huduma kwa wananachi zinaboresha na dhamira ya serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha kwamba fedha za umma zinaelekezwa kwa ajili ya maendeleo.

Fedha zitakazotumika katika uboreshaji huu Shule ni matunda ya kodi za watanzania, narudia tena ni fedha za umma ambazo tunazitoa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watoto wa kitanzania ambao wana safari ya kupata elimu wanapata katika mazingira bora amesisitiza Mstahiki Meya

 Pia Walimu wangu nipende kuwaomba kwani Maudhui ya elimu yapo kwenu hivyo tumieni vyema Taaluma yenu kuwasaidia Wanafunzi hawa ili watakapotoka hapa kwenda Sekondari wawe wenye tabia njema na akili kichwani, ili tusiishie kujenga madarasa na kukarabati shule tu isipokuwa pamoja na kuhakikisha maudhui yanakuwepo mashuleni,Pia endeleeni kuhakikisha Shule yenu inakuwa bora ndani na nje  ya Jiji la Arusha"


Katika hatua nyingine, Mstahiki Meya amemtaka Diwani wa Kata ya Kimandolu Mhe. Abraham Joseph Mollel  kufuatilia kwa karibu matumizi ya fedha hizo zitakazo karabati shule hiyo na kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa.










Share To:

Post A Comment: