Monday, 15 February 2021

WAZIRI UMMY MWALIMU AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA WFP

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu hii leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah Gordon – Gibson katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao wamekubaliana kushirikiana katika jitihada za  kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na uharibifu mazingira nchini kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa chakula.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Bi. Sarah Gordon – Gibson akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Bi. Sarah Gordon – Gibson wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao baina yao kilichofanyika hii leo, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment