Afisa Mawasiliano wa Shirika la Kimataifa Railway Children Africa Henry Mazunda akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani namna wanavyoweza kushirikisha jamii kujua kundi hilo ,jijini Dar es Salaam.
Afisa Saikolojia wa Taasisi  Baba Watoto Asha Salum akizungumza namna anavyofanya kazi na watoto katika kuwajenga kisaikolojia wakiwa wamefika katika kituo cha kufikia, jijini Dar es Salaam.
Afisa Familia wa Taasisi ya Baba Watoto Efransia Kisweka akitoa maelezo wanavyounganisha familia pale mtoto anapotaka kurudi katika familia yake katika kituo cha kufikia Ilala jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano na Utetezi  wa Taasisi ya Baba Watoto Mlwele akizungumza namna wanavyofanya utetezi watoto wanaoishi mtaani pamoja kutoa elimu, jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa Sanaa wa Taasisi ya Baba Watoto Adam Famba akizungumza na  waandishi namna wanavyowafundisha sanaa ,jijini Dar es Salaam.
Mwanaid Salum akizungumza namna alivyounganishwa na mtoto wake aliyetoloka na Taasisi ya Baba Watoto .
Baadhi ya watoto wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Kituo Cha kufikia Watoto wanaoishi na kufanya kazi ,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watoto na Taasisi ya Baba Watoto  wakiwa katika picha pamoja.

*Baba Watoto waweka vituo vya kufikia katika kujua Maendeleo

*Sera za Ulinzi zatakiwa kuwekwa kwa kundi hilo

Na Chalila Kibuda

SHIRIKA la Kimatafa la  Children Railway Africa kwa Kushirikiana na Baba Watoto limesema kuwa Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani hawana uangalizi na kufanya watoto haki kukosa haki nyingi za msingi.

Watoto wa mitaani moja ya haki wanayoikosa afya kutokana na hakuna mtu wa kuweza kuwatowafatilia kwa karibu na hata majanga ya magonjwa ikiwemo la Corona hakuna mtu anayejua watoto hao wanaishije.

Akizungumza na waandishi wa Habari Afisa Habari wa  Railway  Children Africa Henry Mazunda amesema kuwa watoto hao sehemu sahihi ya kuishi ni nyumbani kwao au katika familia zao lakini wametoka kutokana na changamoto mbalimbali hivyo serikali inatakiwa kuweka sera ya ulinzi wa watoto hao.

Mazunda amesema katika mradi waliofanya kwa kushirikiana na Baba Watoto wameanzisha vituo vya kufikia watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ambapo wanaweza kufua nguo, wakapata chakula na hadi matibabu lakini vituo hivyo sio vituo vya kudumu kwao kuishi.

Aidha amesema  kuwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani licha ya kuwa na sehemu ya kufikia wanachowashauri watoto ni pamoja na watoto kuwaunganisha na familia zao na kuwafatilia kwa karibu.

Mratibu wa Mlinzi wa Watoto wa Baba Watoto Tony Mafiye  amesema watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani  wakiwa katika sehemu ya kufikia 'Dropping Center' wamekuwa ni watoto ambao wanajitambua kutokana na mifumo iliyopo katika usimamizi w masuala ya watoto.

Amesema kuwa watoto hao hata wakiwa mtaani asiponekana wanajua jinsi ya kufatilia na hata kama wamekamatwa wanakwenda kutoa dhamana pamoja na kutoa  msaada wa kisheria.

Nae Afisa Mawasiliano na Utetezi wa Baba Watoto Brenda Mlwele amesema kuwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani wakiwa katika vituo vya kufikia wanajifunza vitu mbalimbali ikiwa ni kuwafanya wajisikie jamii inawajali.

Afisa Saikolojia Asha Salum amesema anapokutana na watoto anaongea nao kuangalia namna alivyoathirika kisaikolojia na kutoa ushauri wa kuwajenga upya.

Mwalimu wa Sanaa wa Baba Watoto  Adam Famba amesema kuwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani wanavipaji lakini hata watu hawajui lakini baadhi yao wanaweza kuimba.

Afisa wa Familia wa Baba Efransia Kisweka  amesema kuwa watoto wangine wamewaunganisha na familia zao ambapo wanaendelea vizuri ikiwa pamoja wengine kwenda katika Mafunzo ya ufundi.

Mmoja wa Mama wa Mwenye mtoto aliyetoroka nyumbani Mwanaid Salum amesema anaishukuru Baba Watoto kwa kumuunganisha mtoto wake pamoja na kumjenga kisaikolojia ya kuishi.

Amesema tatizo la mtoto wake lilitokana na familia kumsema kutokana na mtoto huyo alizaliwa nje ya baba ambaye ameolewa na kusema kuwa hata husika katika urithi.

Amesema mtoto huyo anaendelea vizuri lakini hata ndugu wameacha kumsema.

Share To:

Post A Comment: