Mganga mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi amewataka wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza pamoja na yale yasiyo ya kuambukizwa.


Aliyasema hayo leo  wakati akiongoza mazoezi ya pamoja akiwa na watumishi wenzake kutoka Wizara ya Afya ,ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa pamoja na wananchi wa jiji la Dodoma mazoezi yalifanyika katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma.


Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa na mazoea ya kukaa bila kufanya mazoezi jambo ambalo linawasababishia kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara.


"Mazoezi yanasaidia sana  kuondoa magonjwa yasiyoambukiza kama sukari  na presha ,pia huondoa msongo wa mawazo pamoja na kuleta mahusiano baina ya kundi na kundi ,mtu na mtu au na jamii nzima na muunganiko wa kazi kupitia mazoezi hayo"alibainisha Makubi.


Aidha mbali na kufanya mazoezi mganga mkuu  wa Serikali pia alishiriki katika zoezi  la uhamasisha wananchi kufanya usafi kwa kushiriki zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika uwanja wa Nyerere square.



 Akiongea  wakati wa kufanya usafi huo  amewataka wananchi kuimarisha usafi wa mazingira ili  kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.









Share To:

Post A Comment: