Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.

Katibu Mkuu wa wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), , Stella Joel.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Dofa kutoka Karatu ambao wataimba wimbo maalumu kwenye kongamano hilo.



Na Dotto Mwaibale


WANAMUZIKI watakutana  kesho katika kongamano la fursa litakalofanyika Hoteli ya Mont Meru  jijini Arusha.

Mgeni  rasmi  katika kongamano hilo  anatarajiwa  kuwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ambaye atawakabidhi baadhi ya wanamuziki kadi za bima ya afya ya Taifa (NHIF).

  "Wanamuziki watakao pata kadi hizo ni wale ambao wametimiza vigezo kama walivyoeleza Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Eric Kisanga na Katibu Mkuu wa umoja huo, Stella Joel ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo.

Baadhi ya wanamuziki maarufu watakao kuwepo kwenye kongamano hilo ni Emanuel Mbasha (Dsm) Stara Thomas (Dsm) Hafsa kazinja, Rehema Tajiri (Dsm) Edson Mwasabwite (Dsm) 6. Emanuel Mabisa (Dsm)  Rajabu Samatta (Dsm) Goodluck Gozbert (Dsm) Ann Annie (Moshi) Kida Waziri, Agness Lukumay (Karatu) Angel Tango (Mwanza) JCB Makala (Arusha) Renatha Sedekia (Arusha) na Andrew Mnzava (Moshi)

Akiwazungumzia Wanamuziki hao Katibu Mkuu wa TAMiUFO Stella Joel alisema wanaishukuru Serikali kwa kuwakumbuka kuwapatia kadi hizo ambazo zitawasaidia kupata vipimo na matibabu katika hospitali za Serikali na binafsi.

Joel alisema kabla ya hapo wanamuziki wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kushindwa kumudu gharama za vipimo na matibabu.

" Kwa hatua hii iliyochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano hakika wanamuziki wote tunakila sababu ya kuipongeza  kwa kutekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kutusaidia wasanii" alisema Joel.

Rais wa TAMUFO,  Eric Kisanga alisema kongamano hilo ni la kipekee kwani litawahusisha wanamuziki wa kada zote  na kuwa maandalizi yote yamekwisha kamilika.

" Maandalizi yote ya kongamano letu ili la fursa kwa wanamuziki yamekwisha kamilika kwa asilimia kubwa na sasa tupo kumalizia mambo madogo yaliyosalia" alisema Kisanga.

Kisanga alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau wengine kwenye kongamano hilo. 

Share To:

Post A Comment: