Na Heri Shaaban

SERIKALI ya Mtaa Kivule inatarajia kufungua soko la Kivule February Mwaka huu kwa Wafanyabiashara wote wa kata hiyo. 



Akizungumza katika mkutano wa adhara ulioandaliwa na Serikali ya Mtaa Kivule Halmashauri ya Ilala Dar es salaam jana ,Mwenyekiti wa Mtaa Kivule Amos Hangaya alisema alhamisi Febuary 4 Mwaka huu wanawaita Wafanyabiashara wote kwa ajili ya kuwatambua upya pamoja na kugawa vizimba vya Biashara amewataka wafanyabiashara wote kujitokeza siku hiyo. 


Mwenyekiti Amos alisema kwa sasa soko hilo litatumika kwa dhumuni lililolusudiwa soko sio Mnada,Gulio watawatafutia utaratibu kwa ajili ya kuendesha minada yao  kila wiki. 


"Nawaomba Wafanyabiashara wote ambao walipewa vizimba katika soko hili kujitokeza siku hiyo kwa ajili ya kuwatambua rasmi soko linataka kufunguliwa hivyo wote mnatakiwa kufanya biashara sehemu rasmi ambazo zimetengwa na sio mitaani au barabarani " alisema Amos. 


Amos alisema Serikali  ya awamu ya tano TANZANIA ya Uchumi wa viwanda inayoongozwa na Rais John Magufuli inataka wananchi wake wafanye biashara ili wajikwamue kiuchumi sambamba na kuunda viwanda vidogovidogo  ili wapate kipato.



Aliwataka wakazi wa Kivule kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kufanyaji kazi na kuleta maendeleo pamoja na kusimamia miradi ya Serikali ambayo ipo katika eneo hilo.


Wakati huo huo Mwenyekiti Amos alisema moja ya Mikakati yake mingine kuanzisha ruti mpya ya Daladala Kivule Sokoni kwenda Mnazi  Mmoja inatarajia kuanza Wiki hii nauli bei yake shilingi 400/= na ukipanda ufikishwe mwisho wa gari usikubali kushushwa njiani kwa ili wakatishe ruti.


Amos alisema utaratibu wa ruti hiyo daladala hizo umeshakamilika kila abiria akipanda adai tiketi jambo lolote likitokea  atoe taarifa 

Mamlaka husika.


Kwa upande wake Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Kivule Nyasika Getama aliunga mkono juhudi hizo hatawasaidia ili malengo yaweze kutimia 


 Diwani Nyasika aliwataka WANANCHI wa Kata hiyo kukata bima ya afya kwa ajili  matibabu kwani maisha  ya mwanadamu matibabu gharama kubwa hivyo kuna umuhimu wananchi wa kata ya kivule wote wawe na Bima ya afya


Alisema kwa sasa Serikali imerahishisha imetoa Bima iliyoboreshwa kwa ajili ya wananchi wote  kuanzia ngazi ya familia hadi mtu mmoja. 


Akielezea sekta ya elimu alisema kata ya Kivule ipo Ilala Vijijini matokeo ya mwaka  huu shule ya sekondari wamepata alama A ufaulu mzuri na maadili kitaaluma yapo vizuri amewataka wazazi kufatilia maendeleo ya watoto wao na kushirikiana na Walimu wa Msingi na Sekondari.


Mwisho

Share To:

msumbanews

Post A Comment: