Tuesday, 16 February 2021

MRISHO GAMBO ATOA MILIONI 64 ZA MFUKO WA JIMBO KUCHOCHEA MIRADI YA MAENDELEO ARUSHA

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo ametoa Milioni 64,076,000 za Mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo CDFF ili kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Jimboni.


Gambo ameeleza kuwa wamekubaliana na Wajumbe wa Mfuko Jimbo fedha hizo zikatumika katika kuendeleza miundombinu na vivuko katika kata Sita ambazo Kata ya Levolosi wametenga Milioni 20 ili kuboresha Soko la samaki Kilombero.Pia Katika Kata ya Sombetini wametenga Milioni 19 kwa ajili ya Kivuko cha Olamuriaki, Kata ya Osunyai Milioni 10 kutengeneza Kivuko cha JR Kata ya Sakina Milioni 5  Kivuko cha Giriki ,Kata ya Ngarenaro Milioni 5 Kivuko cha Kambi ya Fisi, Kata ya Sinon Milioni 5 Kivuko cha Shinda


Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Arusha Mjini

No comments:

Post a Comment