Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ametoa wito kwa watendaji na viongozi wa Serikali kupanga mipango na miongozo ya maendeleo kuendana na Ilani ya CCM ya mwaka 2020 - 2025.

Ameyasema hayo leo tarehe 16 Februari, 2021 alipotembelea na kukagua maendeleo ya  Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Jijini Dar Es Salaam.

"Mpango wenu, mnaoanisha vema majukumu yenu na ahadi zilizopo kwenye Ilani.  Utaratibu huu umenifurahisha sana, kila jambo mmefanya rejea kwenye Ilani, kama ni mazingira, kama ni haki jinai, maeneo ya milipuko ya magonjwa n.k. Nitoe wito kwa watendaji na viongozi wote wa Serikali  kutumia muongozo wa Ilani katika kupanga mipango ya maendeleo."

Aidha, Katibu Mkuu amefurahishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya kisasa katika Mamlaka hiyo, ambapo amesisitiza umuhimu wa utunzaji wa vifaa hivyo na watumishi kuendelea kufanya kazi kwa uzalendo na uwajibikaji.

Utaratibu huu, ni moja ya Majukumu ya CCM kuendelea kufuatilia kwa karibu utendaji wa Serikali na Mamlaka zake zote katika kuwalinda na kuwaletea maendeleo wananchi.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Share To:

Post A Comment: