Na Ahmed Mahmoud, HAI Mkuu wa wilaya ya Hai,Mkoani Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya amewatoa hofu wananchi wa wilaya hiyo kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kuwataka wasiogope kusalimiana kwa mikono kama ilivyo desturi ya kiafrika kwa kuwa hofu ndio inayokatisha maisha yao. Sabaya ameyasema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la huduma za kinywa na meno wakati akiongea na wafanyakazi wa halmashauri ya Hai ,ambapo alisema ugonjwa wa Corona ni biashara ya watu wachache inayopaswa kuzamwa kwa macho matatu. Alisema kumekuwepo dhana yenye mtazamo tofauti juu ya Kila anayefariki dunia kuelezwa kuwa amekufa kwa Korona Jambo hilo linasababisha wananchi kujawa na hofu na wengi wao kupoteza maisha nakusisitiza kuwa wilaya hiyo ipo salama. Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kujifukiza majani yaliyofukizwa na mungu na kufanywa dawa ya kuwaponya na kuepuka matumizi ya chanjo ambayo ni biashara ya mabeberu na si salama sana. Kwa upande wake naibu waziri wa TAMISEMI,David Silinde aliwataka wananchi kuondoa hofu kwa taarifa za uongo dhidi ya ugonjwa wa Corona Ila wachukue tahadhali za msingi zitakazowaimaisha . Aliitaka jamii kuzingatia maelekezo ya serikali hasa yanayotolewa na Rais John Magufuli kuwa ugonjwa wa Corona unatibika kwa nguvu za mwenyezi mungu . Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya hiyo ,Dkt Irene Haule alisema Jengo hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 82 fedha ambazo Imetokana na mapato ya ndani. Hata hivyo alisema kumekuwepo.na changamoto ya upungufu kwa watumishi wa Afya wilayani humo hasa katika kitengo Cha huduma ya kinywa na meno kwani Kati ya watumishi 10 wanaohitajika kwa Sasa Kuna watumishi watatu tu Jambo ambalo linaleta changamoto kubwa katika utoaji huduma ya kinywa na meno. Ends...
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: