Friday, 8 January 2021

WANANCHI KAPELE MOMBA WALALAMIKA KUNYANYASWA NA WAWEKEZAJI KWA MBUNGE WAO MHE CONDESTA SICHALWE.Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe Condesta Sichalwe ameendelea na ziara zake za kuwasikliza na kutatua changamoto mbalimbali katika Jimbo la Momba. Katika kata ya Kapele Mhe Mbunge aliwasikiliza wananchi wa kata hiyo ambapo moja ya kero iliomkera Mhe Condesta ni kitendo cha wawekezaji kudaiwa kuwanyanyasa wananchi hao mpaka kupelekewa kupigwa


"Nimepokea malalamiko mengi kutoka kwa wanachi wangu wa kata ya Kapele, kunyanyaswa  na baadhi ya watu ambao wanajiita wawekezaji, kwanza wanajimegea maeneo makubwa ya Mashamba bila kufuata utaratibu, halafu wanawageuka wananchi wangu wakikutwa kwenye maeneo hayo wanapigwa na kutishiwa"  Mbunge wa jimbo la Momba Mhe. Condester Michael Sichalwe.


Hata hivyo Mbunge ameahidi kulishughulikia tatizo hilo haraka iwezekanavyo

No comments:

Post a comment