Na Esther Macha,Songwe


SERIKALI mkoani Songwe imemuomba Naibu Waziri wa Maji,Mhandisi Maryprisca Mahundi kufanya mabadiliko ya uongozi wa Mamlaka ya Maji ya Vwawa na Mlowo kwa kukosa ubunifu wa kazi ya kuwapelekea wananchi maji.


Hayo yamesemwa Jana na Mkuu wa mkoa wa Songwe  Breg.Jen Nicodemus  Mwangela baada ya Naibu waziri wa Maji kufanya ziara ya siku moja ya kikazi Mkoani humo ya kukagua miradi ya maji .



"Mamlaka hii bado haijakidhi mahitaji kwa wananchi pamoja na Mhe. Rais, Dkt Magufuli kuleta fedha za kununua pampu kwenye mradi wa Vwawa lakini bado maji wananchi hawapati" amesema Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Mwangela.


Aidhaa, Mamlaka hii ina matatizo ya kutoa bili ya maji mfano Kaya moja inapelekewa bili ya maji ya Shilingi 20,000 au 30,000 kwa mwezi lakini sehemu za kambi kama Jeshi la Polisi na Magereza ambapo matumizi ya maji ni makubwa wanapewa bili ya shilingi 3,000 tu kwa mwezi sasa sisi tunaona uongozi wa Mamlaka hautufai katika kuhudumia wananchi.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi  Mahundi amelazimika kuchukua uamuzi  wa kumsimamisha Kazi Meneja wa Mamlaka ya Maji ya Mji wa Vwawa na Mlowo.


Amesema kuwa mabadiliko makubwa yanakuja katika mkoa wa Songwe ,sekta ya maji inaenda kuwa na.mabadiliko makubwa .


Aidha Naibu waziri amesema kuwa awamu hii ni kazi masuala ya kufanya kazi kwa mazoea hayapo tena ,tunaenda na kasi ya Rais Magufuli.


Mwisho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: