Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Warajis Wasaidizi wa mikoa ya Tanzania Bara leo 6.1.2021 katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi yakiwemo magari pamoja na kompyuta katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Dodoma.

Mrajis Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akitoa taarifa wakati hafla ya kukabidhi vitendea kazi yakiwemo magari pamoja na kompyuta katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Dodoma.

Sehemu ya Warajis kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda leo Jiji Dodoma.

Waziri wa Kilimo Prof.Adolph Mkenda (Katikati) akimkabidhi kompyuta mpakato (laptop)Afisa Ushirika wa Mkoa wa Geita Dorah Mwabeza(Kushoto)kwa niaba ya Mrajis wa Mkoa huo.Prof. Mkenda amekabidhi laptop 20 pamoja na kompyuta za kawaida 50 zilizotolewa naTume ya Maendeleo ya Ushirika leo 6.1.2021 jijini Dodoma kwa warajis.Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege

Waziri wa Kilimo Prof.Adolph Mkenda (Katikati) akimkabidhi funguo za gari Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Simiyu Ibrahimu Kadudu (Kushoto).Prof. Mkenda amekabidhi magari matano yenye thamani ya milioni 275/= yaliyotolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika leo 6.1.2021 jijini Dodoma Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege

Waziri wa Kilimo Prof. Adolph Mkenda (Katikati) akimkabidhi funguo ya gari Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro Henjewele John (Kushoto.

Waziri wa Kilimo Prof. Adolph Mkenda (Katikati) akikimkabidhi kompyuta mpakato (laptop)Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Njombe Bi.Consolata Kiluma (Kushoto).Prof. Mkenda amekabidhi laptop 20 pamoja na kompyuta za kawaida 50 zilizotolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika leo 6.1.2021 jijini Dodoma.Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege

Sehemu ya magari manne aina ya Nissan Hard N 300 Double Cabin 4WD yenye thamani ya Shilingi 275,091,670/- kwa pamoja yalikabidhiwa kwa Warajis Wasaidizi wa mkoa wa Simiyu, Kilimanjaro, Njombe na Dar es Salaaam na gari moja lililotumika kwa mkoa wa Kigoma.

Na Alex Sonna, Dodoma 

SERIKALI imeahidi kuendelea kutatua changamoto ya vitendea kazi kwa watumishi Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini(TCDC) ili wafanye kazi kwa ufanisi na kurejesha hadhi na heshima ya ushirika nchini. Sambamba na hilo, imeapa kutofumbia macho mtu yeyote atakayebainika kuchezea fedha za ushirika. 

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda hafla ya kukabidhi magari matano na komputa 70 kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi kwa watumishi wa Tume hiyo.

  Amesema anafahamu watumishi hao wanafanya kazi kwenye mazingira magumu hivyo serikali inapambana ili kuhakikisha wanaondoa kero zinazowakabili. 

 Hata hivyo, ameeleza bado kunahitajika mapambano ya wizi na ubadhirifu kwenye vyama vya ushirika licha ya kuonekana kupungua kutokana na jitihada zilizofanywa na serikali za kurudisha mali za ushirika. 

"Hatutachekeana na mtu anayecheza na mali za ushirika kwasababu ukifanya hivyo unakatisha watu tamaa, watakuwa hawana hamu ya kujiunga na ushirika, Warajis Wasaidizi tusimame kidete kwenye hilo,"amesema.

  Pia amesema licha ya ubadhirifu kupungua lakini bado kuna tatizo la vyama kushindwa kuandaa vyema hesabu zake na kusababisha kukosa hati safi. Kuhusu Sheria, Waziri huyo amesema kuna kazi ya kurudisha imani za watu kwenye ushirika kwa kupitia upya Sheria ya Ushirika na tayari kazi imeshaanza. 

 Awali, Mtendaji Mkuu wa Tume hiyo ambaye pia ni Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk.Benson Ndiege, amesema Tume itaendelea kupambana na kero zinazoukabili ushirika ikiwamo ubadhirifu na uongozi mbovu kwenye vyama hivyo.

  Aidha, Dk.Ndiege amesema Tume ipo kwenye mpango wa kuimarisha ofisi za ushirika nchini na itahakikisha kila mkoa una gari kabla ya mwaka wa fedha 2020/21 kukamilika.  

"Leo kwa kutumia mapato ya ndani Sh.Milioni 275 zimenunua magari manne ambayo yataenda kwa Warajis wa mikoa ya Dar es salaam, Simiyu, Kilimanjaro na Njombe na pia tutatoa gari moja kwenda Kigoma kutokana na umuhimu wa kilimo cha michikichi,"amesema.

Aidha amesema wamegawa komputa 70 ambapo kati ya hizo 20 ni komputa mpakato(laptops) ambapo komputa 50 zimetolewa na Benki ya CRDB na hizo zingine zimenunuliwa kwa mapato ya ndani.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: