Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini ambae pia ni Waziri (OMR) Muungano na Mazingira leo  tarehe 2 januari 2021 amegawa mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 8.4 katika shule 5 za Sekondari Jijini Tanga ambazo wanaendelea na ujenzi wa madarasa ili kuwezesha watoto wote waliofaulu kuanza kidato cha kwanza mwezi huu.


Shule zilizopata mifuko ya saruji kutoka kwa Mhe Mbunge ni Pongwe Sekondari (Pongwe), 

MACECHU Sekondari (Chumbageni), Mikanjuni Sekondari (Mabawa), Japan Sekondari (Tangasisi) na Mnyanjani Sekondari ya Kata ya Makorora. 


Wakati akikabidhi saruji hizo, Mh.Ummy Mwalimu pia amewataka Wakuu wa Shule na Kamati za shule kuzingatia Miongozo ya Serikali katika kuwachangisha fedha wazazi wa wanafunzi wanaonza kidato cha kwanza.


Ameeleza kuwa endapo kuna ulazima wa kuchangisha wazazi kwa ajili ya wanafunzi hao ni lazima suala hilo kujadiliwa na kukubaliwa na Wazazi/Walezi wenye watoto katika shule husika.


Wakipokea mchango huo wa Mbunge, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe Abdurahman Shiloow, Madiwani wa kata husika na Mkurugenzi wa Jiji wamemshukuru Mh Ummy kwa mchango wake mkubwa katika kuwezesha ujenzi wa madarasa na kuwa wataendelea kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake ya kibunge.

Share To:

Post A Comment: