NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Baraza la madiwani jiji la Arusha limeanza kuwatumikia wananchi huku likiendesha vikao kwa kutumia teknolojia ya Vishkwambi(Tablet) badala ya kutumia makabrasha kama ilivyokuwa katika mabaraza yaliyopita.


Wakizungumza na waandishi wa habari badhii ya madiwani baada ya kumalizika kwa semina elekezi iliyotolewa kwa madiwani hao kwa muda wa siku tatu ikiwa ni pamoja na kila mmoja kukabidhiwa kifaa chake(vishkwambi) kwaajili ya kuanza kazi rasmi walisema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kutatua changamoto zilizokuwepo awali.


Naibu Meya wa jiji hilo Veronica Moilange alisema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kupunguza matumizi ya fedha zilizokuwa zikitumika kuchapisha makabrasha katika vikao vyote vya baraza na kila inapotokea taarifa mpya ambapo fedha hizo kwa sasa zitaelekezwa katika shughuli nyingine ya kimaendeo ndani ya jiji.


Alisema kuwa  pia Vishkwambi  hivyo vitasaidia kutatua changamoto ya mafiwani kuchelewa kupata taarifa kwani mahali popote atakapokuwa diwani atapata taarifa kwa wakati na kutekeleza wajibu wake.


"Hivi vifaa vimekuwa vya muhimu sana kwetu kwani gharama za machapisho zimeondoka lakini hakuna diwani atayechelewa au kukosa taarifa yoyote ikiwemo agenda za mikutano yetu tutapata kwa wakati na tutazipitia bila kuwa na yoyote atayeshindwa kushiriki vikao ipasavyo kwa kukosa taarifa kwa wakati," Alisema Naibu Meya wa jiji la Arusha.



Diwani wa kata ya Sekei Gerald John Sebastian alisema kuwa jiji la Arusha linaweza kuwa namba moja kwani kwasasa watatekeleza wajibu wao kwa kutumia teknolojia  ambayo itasaidia kupunguza matumizi ya fedha pamoja na kila mmoja wao kupata taarifa ndani ya dakika moja na sio kusubiri kusambaziwa makabrasha katika ofisi zao.


"Kwa kutumia teknolojia ipasavyo tunaweza kufanya mabadiliko makubwa katika utendaji wetu wa kazi kwani hii itatusaidia kupata taarifa mbalimbali kwa wakati lakini pia kuwasilisha kwenye baraza changamoto za wananchi wetu kwa haraka na kupata ufumbuzi," Alisema Diwani Sebastian.


Isaya Doita diwani kata ya Ngarenaro ambaye pia ni diwani aliyepata nafasi hiyo kwa awamu wa tatu sasa alieleza kuwa awali katika mabara yaliyomaliza muda wake kulikuwa na changamoto ya madiwani kuchelewa kupata taarifa na wakati mwingine kutokupata kabisa lakini hivi sasa kwa kuwa watafanya kazi kupitia teknolojia zaidi  anaamini wote watapata taarifa kwa wakati na ushiriki wa maendeo utakuwa mkubwa zaidi.


"Kupitia teknolojia hii tukishirikiana vizuri tutaweza kutatua kero za wananchi bila hata kukutana katika vikao kwani tutakuwa tayari wakati wote kwani awali ilikuwa ngumu kusafirisha makabrasha  na muhusika kuipata kwa wakati pamoja na kupeleka hoja yake juu ya agenda zilizopo kwa wakati,"Alisema Diwani Doita.


Aidha  kutoka kana na semina elekezi waliyoipata walisema kuwa wamepata uelewa wa mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna watavyofanya kazi zao kwa kufuata taratibu ma sheria, kushirikiana badala ya kuwa na malumbano pamoja na uwezo mkubwa wa kufanya kazi na kuleta mabadiliko.


Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega  akifunga semina hiyo alisema kuwa matumizi ya vishkwambi hivyo vitawasaidia kuokoa muda kwani wote watapata document  kwa wakati bila kujali mahali alipo mtu.



Sambamba  na hilo pia Kwitega aliwataka kuzikatia mahusiano kati yao, wataalamu na wananchi, pamoja na kujenga ukaribu utakaofanya wawe ma agenda moja na sio kuwa na migogoro itayokwamisha  kusukuma maendeleo mbele.


"Watumieni wananchi kujua changamoto zilizopo, wataalamu kusukuma maendeleo mbele lakini pia na nyie mshirikiane  katika kufanya shughuli zote kwa manufaa ya wananchi wa jiji la Arusha na nchi kwa ujula," Alisema.



Naye Mkurugenzi wa jiji hilo Dkt John Pima alisema kuwa kwa muda wa siku tatu madiwani hao wameweza kujifunza mada 11 zitakazosaidia kuboresha namna watakavyoenda kufanya kazi na kunufaisha jamii.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: