Friday, 1 January 2021

KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS YAHIMIZA UBUNIFU KWA WAFANYAKAZI WAKENa Ferdinand Shayo,Manyara.


Kampuni ya Mati Super Brands Limited iliyoko Mkoani Manyara imewataka Wafanyakazi kufanya kazi kwa umoja na mshikamano huku wakiongeza Ubunifu kazini ili kuongeza tija na ufanisi .


Mkurugenzi wa kampuni hiyo David Mlokozi akizungumza katika Mafunzo Maalumu ya "Team Building" yaliyowakutanisha Wafanyakazi wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbali mbali ,Mlokozi amesema kuwa Ubunifu Ni Jambo muhimu kazini  linasaidia katika kubuni bidhaa mpya.


Mlokozi amesema kuwa Lengo la kuandaa tukio Hilo ni kuhimiza ushirikiano na mshikamano kwa Wafanyakazi wa idara zote ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.


Meneja Rasilimali watu wa Kampuni hiyo Doreen Raphael amesema kuwa Mafunzo hayo yanasidia kuwaweka Wafanyakazi pamoja na kujenga umoja Kama taasisi.


Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Gwandumi Npoma  pamoja Meneja Uzalishaji wa Kampuni hiyo Gasper Mlay amepongeza utaratibu wa Kampuni hiyo kwani unalenga kujenga motisha kwa wafanyakazi na unapaswa kuigwa na makampuni mengine.


Mafunzo ya Team Building yameambatana na michezo mbali mbali Ikiwemo mpira wa miguu,kukimbiza kuku,kucheza muziki na mwisho zawadi zilitolewa kwa washindi wote  .

No comments:

Post a Comment