China imeanza kutumia aina mpya ya kuchukua sampuli za kipimo Cha Corona kupitia sehemu ya haja kubwa.

Mamlaka zinasema aina hii ya kipimo ni ya kuaminika zaidi na haraka.

Kipimo hiki kinahusisha kuingiwa kwa kifaa maalumu chenye pamba kama sentimita 1 ama 2 katika njia ya haja kubwa kisha kutoa sampuli ambayo itatumika kuangalia uwepo wa virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa televisheni ya taifa hilo CCTV inasema kuwa aina hii ya kipimo itatumika kwa visa vitakavyo hitaji uangalizi wa hali ya juu.

Watu ambao watapimwa na kipimo hiki ni pamoja na abiria watakaoingia Beijing na watu watakaokuwa wamewekwa karantini.

“Kipimo hiki kina ufanisi zaidi kuliko kile Cha puani na kwenye koo” Anasema Li Tongzeng afisa msaidizi katika kitengo Cha mfumo wa upumuaji katika hospitali ya You an.

Hatua hii inakuja kama maandalizi ya kupambana na Corona wakati wa sherehe za mwaka mpya wa China

Share To:

Post A Comment: