Sunday, 27 December 2020

ZIARA YA MWAMBE YABAINI MBONDE SIO KITUO CHA AFYA

 


Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini akiambatana na Madiwani wote wa Halmashauri ya Mji Leo tar 26 Des, 2020 wamefanya ziara kwenye Hospitali ya Mkomaindo na Mbonde. 


Mheshimiwa Waziri akiwa Mkomaindo, amekagua ukarabati wa chumba cha kuhifadhia dawa kama ambavyo aliagiza alipofanya ziara wiki chache zilizopita.


 Katika ziara hiyo ametoa agizo kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji kuwa, ni marufuku akina mama wajawazito kulipa fedha wakati wa kujifungua. 


Pia ametoa agizo kuwa Duka la Dawa lililopo hospitalini hapo, lisimamiwe na Halmashauri ya Mji na sio hospitali ili iwe rahisi wateja kupata huduma hiyo kwa uhakika.


 Sambamba na agizo hilo Mheshimiwa Waziri ametembelea Mbonde ambako tangu awali panafahamika Kama Kituo cha Afya cha Mbonde na ameshangazwa kusikia kuwa na Mbonde imesajiliwa Kama Zahanati na sio Kituo cha Afya.


 Lakini pia, kipekee amempongeza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Salumu Gembe kwa namna anavyojitahidi kuleta mabadiliko hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment