Friday, 4 December 2020

WATAKIWA KUFUATA SHERIA

 Na Woinde Shizza , ARUSHA

 Wito umetolewa kwa wataalam wa ununuzi na  ugavi  kufuata sheria kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuweza kukuza uchumi wa  nchi yetu.


Hayo yamebainishwa na  mkuu wa idara ya ununuzi kutoka shirika la umeme Tanesco Nyalu Patson  Mwamwaja wakati akiongea na waandishi wa habari Mara baada ya kupokea hati ya shukrani ya kuthamini mkutano wa 11 ununuzi na ugavi uliofanyika katika ukumbi wa AICC uliopo mkoani Arusha


Alisema kuwa vyema wakaacha uzembe  na wafanye kazi kwa  weledi katika kusimamia mnyororo wa ununuzi na ugavi iliwasikwamishe utekelezaji wa miradi. 


 Alisema kuwa wameamua kuthamini kongamano hilo kwakuwa wao ni wadau wakubwa na shirika hilo kunatoa mchango mkubwa Sana katika fani hii ya ununuzi na ugavi


Alisema shirika la Tanesco ndilo linaloongoza kwa kuajiri wanunuzi wengi na wagavi ,ambao ni wafanisi na wanaoleta Maendeleo katika ufanisi endelevu wa nchi na wa fani hii kwa ujumla ,na waendelee kufanya kazi vyema kwa ajili ya Maendeleo ya nchi yetu.


Aliwataka waendelee kufuata sheria  kanuni za maadili na kuendelea  kutoa ushauri wa manunuzi kwa  kufuata  Sheria ya manunuzi ya umma .


No comments:

Post a Comment