Mkuu wa wilaya ya Arusha Kennan Kihongosi amepiga marufuku watu wote wasio wazalendo katika kulinda na kutunza rasilimali za nchi kwani serikali itachukua hatua kali dhidi yao pasipo kuwachea wala kuwaonea huruma.


Kennan alitoa marufuku hiyo wakati akifafanua juu ya viboko alivyowachapa wanafunzi na vijana walihusika katika tukio la wizi viti 108 vya kukalia wanafunzi katika shule ya sekondari Sinoni iliyopo katika wilaya hiyo baada ya baadhi ya watu kuhoji ni kwanini alichukua hatua hiyo.


Alisema hakuna sababu ya kufurahia watu wachache wanaohujumu miundombinu kwa tamaa zao binafsi na kusababisha watoto 108 kukosa viti vya kukalia ili kuweza kusoma,kupata elimu ikiwa ni pamoja na kunufaika na sera ya elimu ambayo serikali ya inawapatia.


“Serikali inagharamia fedha nyingi zaidi ya bilioni 24.4 kila mwezi  kwaajili ya elimu bure na imeweka miundombinu ya madarasa lakini watanzania wengine waliokosa uzalendo wanawatuma watoto waende kuiba miundombinu hiyo, kwa gharama ya shilingi miatano alafu anatokea mtu anawatetea hii haikubaliki,” Alisema Kennan.


Alieleza kuwa serikali imelikataa jambo hilo, na haitaweza kulikubali bali watazidi kuchukua hatua kali kwa wale watakaobainika kuhujumu miundombinu ya shule kwa tamaa zao binafsi zitakazoleta madhara kwa wanafunzi kushindwa kupata elimu ipasavyo.


“Utaona mtu mzima mwenye akili zake timamu kabisa ananunua kiti chenye muhuri wa shule na kukivunja kisha anakwenda kupima chuma chakavu ili aweze kupata fedha, kiti chenye thamani ya shilingi laki moja kinauzwa shilingi mia tano hii haikubaliki,”Alieleza.


“Mimi niliwaadhibu kama mzazi kwani mzazi yoyote ambaye angeona tukio lile lazima moyo ungemuuma kama kweli anawapenda watoto wa Tanzania kwani miaka kadhaa iliyopita kulikuwa uhaba mkubwa wa madawati na watu wote mnalifahamu hili, serikali ilichukia jitihada ikachonga madawati nchi nzima alafu leo mtu mmoja au watano wanakwenda kuhujumu kwaajili ya shilingi 500,”Alifafanua.


Aidha Kenan aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kila mmoja atambue kuwa mali za serikali ni mali za uuma hivyo  washikamane na serikali yao kuhakikiaha wanalinda na kutunza kwa mslahi mapana ya nchi.


Hata hivyo mnamo December 16 katika wilaya hiyo walikamatwa wanafunzi wa tatu wa shule hiyo ambao walichapwa viboko vitatu kila mmoja na kuzuiwa kuhudhuria masomo hadi gharama za viti hivyo vitakapolipwa lakini pia walikamatwa vijana 5 ambao wanne waliadhibiwa viboko vitatu kila mmoja na ambapo wote walipelekwa rumande.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: