Wednesday, 9 December 2020

UPATIKANAJI WA UHAKIKA NA BEI KUBWA ZA CHANJO CHANZO CHA WAFUGAJI KUSHINDWA KUCHANJA MIFUGONA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Kukosekana kwa upatikanaji wa uhakika na haraka wa chanjo za mifugo pamoja na bei kubwa ya chanjo hizo kumetajwa kuwa ndio changamoto kubwa kwa wafugaji wengi kushindwa kuchanja mifugo yao.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa huduma ya afya ya mifugo Tanzania Prof Ezron Nonga wakati akizungumza na maafisa ughani katika Mkutano wa 16 wa Tavepa uliofanyika mkoani Arusha ukiwa na kaulimbiu isemayo "Wanyama wenyewe afya ni fahari kwetu kuelekea uchumi wa viwanda".

“Wafugaji nchini wanakabiliwa na tatizo la kupata chanjo za mifugo yao Kwa wakati ili kukabiliana na magonjwa ya mifugo kakini pia bei kubwa ya chanjo ambazo wafugaji wanashindwa kuzimudu” Alisema Profesa Nonga


Kwaupande wake Mwenyekiti wa TAVEPA Salim Msellem aliwatoa wasiwasi wafugaji kuhusu chanjo zinazotengenezwa hapa nchini kuwa zimefuata taratibu zote zinazotakiwa hivyo wazitumie kuliko kuhamini za nje zaidi.

“Niwaombe  wafugaji  mtumia chanjo zinazotengenezwa nchini kwani zimekidhi vigezo msiwe na wasiwasi nazo ni nzuri na bora na endapo mtatumia mtakuwa mashuhuda kueleza jinsi zinavyofanya kazi”Alisema.Naye mwezeshaji wamafunzo hayo Dk Peter Makang'a alitoa wito kwa washiriki wa semina hiyo kutumia vizuri mafunzo hayo kwa faida ya watanzania wote ili kuleta tija  kwa wafugaji na kukuza uchumi wa nchi.


Dativa Kimolo ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo alisema wanashukuru kwa kupata mafunzo hayo kwani wataweza kuwa mstari wa mbele katika kuwaelimisha wafugaji kufuata sheria na kuona umuhimu wa chanjo kwani ni suala la lazima na si hiari .

No comments:

Post a Comment