Tuesday, 8 December 2020

RC ARUSHA; MNAMWAKILISHA RAIS KATIKA MIRADI MNAYOISIMAMIA

 


NA NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA 


Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Kimanta amewataka wataalamu wa manunuzi kutambua katika miradi wanayosimamia waserikali hivyo wanawajibu mkubwa wa kuhakikisha miradi hiyo inafanikiwa.


Kimanta aliwaeleza  hayo wakati akifunga kongamano la 11 la wataalamu hao ambapo alisema fedha zinazotumika kutekeleza miradi hiyo ni fedha za kodi  wananchi na hata ikiwa ni msaada kutoka nje inaletwa kwaajili ya watanzania na mahusiano yaliyopo hivyo akikisheni hamuikwamishi serikali.


"Mnapofanya vibaya watu hawatajenga chuki na nyie bali na mfumo nzima wa serikali na hata kwenye misaada  kosa Laki wewe mtu mmoja tu linaweza kuharibu mahusiano ya nchi na nchi,"Alisema Kimanta.


Alieleza kuwa gani ya ununuzi na ugavi ni jukumu lao kuhakikisha nchi inakuwa katika uchumi wa viwanda hivyo wanahitajika  wataalamu wenye sifa stahiki, nidhamu ya kazi, uzalendo, maadili na weledi wa hali ya juu.


"Nina imani kuwa mnajua malengo na mikakati ya serikali ya awamu ya tano katika kukuza viwanda na katika kuusimamia hili akikisheni mnatimiza wajibu wenu mnapokuwa katika maeneo yenu ya kazi," Alisisitiza.


Alifafanua kuwa kwa yoyote atakayefanya hilaza kukwamisha juhudi za serikali hatafumbiwa macho wala kuonewa huruma na kwa kuchukuliwa  hatua za kisheria na kupewa adhabu itasaidia kuleta nidhamu ya kazi.


Aidha alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya waajiri hapa nchini wanaoajiri watu wa ununuzi na ugavi ambao hawajasajiliwa na bodi na haijulikani wanatumia vigezo gani kuwaajiri jambo ambalo kisheria ni kosa kwani anakiuka sheria ya bodi ya ya wataalamu namba 179.


"Ni kosa kubwa kuajiri mtu wa manunuzi na ugavi  ambaye hajasajiliwa naagiza bodi mchukue mchukue hatua za kisheria na mnaposimamia  sheria msione huruma kwani waliosajiliwa wana vitu vya ziara,"Aliagiza.


Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa  PSPTB  Godfrey Mbanyi katika mkutano huo wamejadili jinsi kuusimamia na kuweza kuboresha ili kuweza kufikia ubora wa hali ya juu katika usimamizi wa mnyororo wa manunuzi na ugavi.


"Tulioyajadili tumeyachukua na yawasaidia kuboresha taaluma na taasisi kwa ujumla," Alisema Mbanyi.


Hata hivyo aliwataka wataalamu hao kufanya kazi kwa bidii ili waweze kufanikisha nchi katika maendeleo ambayo Rais amekusudia.

No comments:

Post a Comment