Na Heri Shaaban
MBUNGE wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu Leo ametatua kero ya kufunga Barabara Mtaa wa Maliki Upanga Wilayani Ilala.
Akizungumza wakati wa kutatua kero hiyo Zungu alisema kufungwa kwa barabara hiyo kumekwamisha shughuli za uzalishaji kiuchumi kutokana na Barabara hiyo kubwa inaunganisha mawasiliano Muhimbili ambapo kwa sasa magari yanazunguka umbali mrefu.
Katika ziara hiyo Mbunge wa Ilala Zungu aliongozana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri, Wataalam WA TARURA na Mhandisi wa manispaa ya Ilala.
"Mkandarasi wa ujenzi wa Dawasa miundombinu ya DAWASA alifunga barabara hii ya maliki mda mrefu tunaomba uharakishe ujenzi Barabara iweze kutumika " alisema Zungu.
Zungu alisema kufungwa kwa Barabara hiyo kumepelekea wafanyabiashara kukosa wateja wao wa kila siku
Zungu alimpongeza Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala kwa kutatua kero hiyo ambapo Mkurugenzi wa Ilala ametoa siku tatu Mkandarasi wa miuondombinu ya DAWASA kampuni ya BUCICO awe amefungua njia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri amezitaka Kampuni za ujenzi pindi wanapoomba tenda mbalimbali kuzingatia utaratibu na sheria za ujenzi.
Katika ziara hiyo Mbunge Musa Zungu aliongozana na Watalaam wa TARURA ,Mhandisi wa manispaa ya Ilala na Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto
Mkandarasi wa miundombinu ya DAWASA kampuni ya BUCICO Yuda Maseru alisema Jumatano Desemba 30/2020 Barabara ya Mtaa Maliki iitafunguliwa.
Mwisho
Post A Comment: