Wednesday, 23 December 2020

MBUNGE MAVUNDE AZINDUA KISIMA CHA MAJI HOMBOLO NA KUCHANGIA UJENZI WA SHULE YA MSINGI MPYA

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amezindua kisima cha Maji katika Mtaa wa Ngh'ole-Mkoyo,Hombolo Bwawani ikiwa ni muendelezo wa ufadhili kutoka Taasisi ya Pole Pole ya Alessandria,Italia iliyowakilishwa na Makamu Askofu wa Jimbo kuu Dodoma Padri Onesmo Wissi ambaye alionesha utayari wa Taasisi husika kushirikiana na Mbunge Mavunde katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii katika Jimbo la Dodoma Mjini.


"Kisima hichi kitahudumia zaidi ya wananchi  4000 ambao awali walikuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa Maji.Hivyo ni vyema kuhakikisha mradi huu unalindwa na kutunzwa ili ulete manufaa yaliyokusudiwa kwa Wananchi"Alisema  Mavunde


Kisima hichi kinatimiza idadi ya visima 8 kati ya 20 vilivyoahidiwa kuchimbwa na Mbunge Mavunde katika Jimbo la Dodoma Mjini mara baada ya kuchaguliwa.


Wakati huo huo Mbunge Mavunde ameunga mkono jitihada za Wananchi kwenye ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Ngh'ole kwa kuchangia matofali 1000 na mifuko ya saruji 130

Akishukuru kwa niaba ya Wananchi,Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani Mh.Assedi Ndajilo amewataka wananchi wa Ngh'ole kuutunza mradi huu wa Maji na kutoa taarifa iwapo itajitokeza hujuma juu ya mradi husika na serikali ya kata itakuwa tayari muda wote kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo ya maji bila vikwazo.

No comments:

Post a Comment