Wednesday, 23 December 2020

Jafo aridhishwa miradi ya mendeleo Mkoani RuvumaNa. Angela Msimbira SONGEA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Mhe. Selemani Jafo  ameridhishwa  na utekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya  Songea, Mkoani Ruvuma


Akikagua miradi ya maendeleo leo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manispaa ya Songea Mkoani Waziri Jafo  amesema  miradi iliyotekelezwa katika Halmashauri hiyo   imesimamiwa  kwa weledi na viwango vinavyohitajika na Serikali


“Nimeridhishwa na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kuwa imesimamiwa kwa weledi mkubwa  na  imejengwa kwa viwango ninavyoridhisha,” ameseisistiza waziri Jafo


Amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanaimarisha ulinzi  na  kutunza  miundombinu hiyo iliyojengwa kwa gharama kubwa ili miundombinu hiyo idumu kwa muda mrefu.

Akifafanua zaidi wakati akiongea na wanachi wa Kata ya Majengo

 

Waziri Jafo amesema Mji wa Songea kipindi cha nyuma kulikuwa  na  miundombinu mibovu , hata hivyo Serikali ya awamu ya  awamu ya Tano  iliweza kujenga  barabara kwa kiwango cha lami  katika manispaa, Miji , majiji na Halmashauri.


Amesema kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi inaendelea kufanya tathmini  ya miradi ambayo itaweza kutekelezwa katika kipindi kingine cha miaka mitano, hivyo ujenzi mwingine wa miundombinu utafanyika  ambapo  kwa sasa  kuna mpango wa kuboresha miundombinu   katika miji  45 


Aidha Waziri Jafo ametembelea stendi ya mabasi uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.887 machinjio ya kisasa pamoja na barabara yenye urefu wa kilometa 10 zilizojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 13.548 katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

No comments:

Post a Comment