Naibu waziri wa afya jinsia wazee na watoto, Dr Godwin Mollel amesema  kuwa hosipitali ya rufaa ya Mauntmeru sio wakala wa hosipitali binafsi hivyo madaktari waache tabia ya kuwaelekeza wagonjwa kwenda katika hosipitali binafsi wakati uwezo wa kuwahudumia wanao.


Dr Mollel aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa hosipitali hiyo  katika ziara yake ambapo alisema kuna baadhi ya madaktari wasio waadilifu  ambao badala ya kuwahudumia wagonjwa  wanawaelekeza katika vijiwe vyao jambo linalochafua sifa ya hisipitali ikiwa ni pamoja na husipitali kukosa mapato.


"Siwakatazi kuwa na vijiwe lakini nataka muwe waadilifu na mtimize wajibu wenu hapa, na sio kuelekeza wagonjwa sehemu nyingine wakati uwezo wa kuwahudumia  upo mnaharibu hosipitalina kukosesha mapato," Alisema Dr Mollel.


Aidha alisema kuwa pamoja na changamoto hiyo pia ana ushahidi wa mtoto wa chini aliyemulikwa na mionzi (X-ray) katika hosipitali hiyo lakini baada ya kugundulika kuwa amefunjika alikataliwa kutibiwa hadi ilipwe shilingi laki moja na nusu  jambo ambalo sio sawa na mgonjwa huyo kwenda kutibiwa kwa shilingi elfu 56 katika hosipitali ya Mkwaranga.



Alisema kuwa pamoja na changamoto hiyo pia kuna wizi mkubwa unaofanywa na watumishi katika hosipitali hiyo ikiwemo watu wa mahabara, famasia na wengine wengine na kutolea mfano kuwa analo fail la mgonjwa ambaye alitakiwa kulipa shilingi laki saba za matibabu za matibabu kwa muda aliokuwepo lakini muhudumu akanwambia alipe laki mbili na alipompa alimruhusu bila kujali malipo ya hosipitali.



 “Pamoja na hospitali hii ya rufaa ya mkoa kuongeza mapato kutoka sh.milioni 200 hadi 361 bado kuna mambo mabaya yanaofanywa na baadhi madaktari wa kwa wagonjwa washindwe kupata huduma na waende katika hospitali zao binafsi”Alisema



Alisema asilimia 75 ya matatizo yaliyopo kwenye afya yanatokana na utendaji mbovu unaofanywa na baadhi ya madaktari  kutokana na ukosefu wa uadilifu kwa wataalamu wa afya ambapo husababishia baadhi ya watendaji wazuri kuteseka kwasababu ya watu wachache wanaotumia hospitali za serikali kama vijiwe


Awali akisoma taarifa ya hospitali hiyo,Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mountmeru mkoa wa Arusha,Dr Alex Ernest alisema hospitali hiyo inahudumia watu zaidii ya milioni 2 ndani na nje ya viunga vya mkoa huo ikiwa wagonjwa wa nje ni kati ya 320 hadi 540 kwa siku na wa marudio 250 hadi 350,wapya 60 hadi 120 na watoto kati ya 30 hadi 50 kwa siku.


Mganga mfawidhi alisema wagonjwa wanaolazwa ni kati ya 70 hadi 120 ,wananojifungua ni 15 hadi 40 kwa siku ,waliojifungua kwa upasuji ni kati ya 5 hadi 15 lakini pamoja na hayo hospitali hiyo inakabiliwa na uhaba wa vifaa,uchakavu wa majengo,vyumba vya upasuaji,upungufu wa watumishi 232 walipo 451 ikiwa uhitaji ni 683.


"Majengo chakavu yamepelekea kuwa na miundombinu mibovu ya maji na umeme hali inayosababisha kuwa na bili kubwa hata hivyo hospitali inashughulikia hili swala na kuunda timu ndogo ya miundombinu hiyo ili kuweza kuona namna.ya kupunguza gharama hizo,"alisema Mganga Mfawidhi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: