William Peter Ndilla 

Sumve.Mwanza

November 15,2020.


Sijui kama Wabunge wetu wateule na Bunge la kumi na mbili la Job Ndugai wanajua kuwa hotoba ya Mh.Rais ya kulifungua Bunge ilikuwa inawahusu wao kwanza zaidi labda kuliko mtu mwingine.


Rais John Pombe Magufuli ameshatimiza wajibu wake kwa kutoa dira ya miaka mitano ya Serikali yake na sasa ni wajibu wa kila kundi kutafsiri hotuba husika na kuchukua hatua kwa makusudi ya kutekeleza dira hiyo.


Baada ya kumsikiliza Mh.Rais juzi,jana na leo nilijipa mda wa kuitafsiri hotuba ile ili kuweza kujua nani anawajibu gani,katika eneo gani na lini.


Ni muhimu sana kwa kila kundi kuanza kuitafsiri ili kila taasisi,sekta,idara na mtu mmoja mmoja kujua mchango wake utakuwa upi katika kutelekeza dira ya Serikali ya miaka mitano.Ni muhimu sana!


Wajibu wa Serikali ya awamu ya tano unaendelea kutimizwa kufikia dira husika na ndio maana Rais katika hotuba yake ya juzi, alirejea sana hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la kumi na moja mwaka 2015.


Kwahiyo anachotaka kusema Mh.Rais ni kwamba kazi aliyoianza mwaka 2015  bado inaendelea zaidi anachoitaji ni taasisi zingine kama Bunge kumuunga mkono.


KAZI YA SERIKALI YA JPM TANGIA 2015 MPAKA 2025 NI HIPI?


Kazi kubwa ya Serikali ya awamu ya tano ilikuwa moja tu nayo ni "To Break Country Cycle of Poverty" yaani kubomoa ukuta wa umasikini wa Taifa.


Serikali ya awamu ya tano ilishakuja na kauli mpya masikioni mwa watu".....Nchi hii ni tajiriii....."amesikika mara kwa mara Rais akisema.Wajibu wake mkubwa ilikuwa kuwathibitishia Watanzania kuwa Nchi hii"Tanzania" ni tajiri.


Safari ya kuifikia Tanzania tajiri ilianza kwa JPM kuja na Mpango mageuzi ya kiuchumi kwa kuzitambua na kufufua sekta Mkakati za kiuchumi"Economic Base Diversification" kuelekea Tanzania tajiri.


Kwa mujibu wa wataalam wa mambo ya "Public finance" wanasema,utambuzi wa muundo uchumi gani unapaswa kutengeneza katika Nchi yako unategemea sana aina ya utajiri wa rasilimali,giografia yako pamoja na rasilimali watu uliyonayo katika Taifa.


Uanzishaji wa miradi ya kimkakati kama SGR,Ununuzi wa Ndege,Meli,uendelezaji wa Miundombinu ya barabara,upanuzi wa Bandari,Marekebisho ya sheria za madini,elimu bure na mengine mengi ni sehemu ya mpango wa kuvunja ukuta wa umasikini"Economic Diversification Strategy".


Serikali ya awamu ya tano ilifanya kazi hiyo kwa Weledi mkubwa mpaka katika maeneo ya kubadili sera, sheria na kutoa maelekezo kwenya baadhi ya Maeneo"Wamachinga Wauze Bidhaa zao Popote".


Wakati hotuba ya juzi ikishangiliwa na watu wa kada mbalimbali kwa kugusa maeneo muhimu yote ambayo Serikali inataka kupeleka nguvu kama Kilimo,Uvuvi,Ufugaji,Michezo,Sanaa,Utaliii,Madini,Biashara na mengineyo bado haitoweza kufanikiwa kama taasisi zingine zitashindwa kujua wajibu wao katika kutekeleza dira ya Serikali ya miaka mitano.


JE, BUNGE LA KUMI NA MBILI LINAJUA KUWA NDILO LINABEBA"MSALA" MZIMA?


Wajibu wa Bunge kama ulivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni kuishauri Serikali pamoja na kutunga Sheria pamoja na mambo mengine.


Bunge la kumi na mbili litakuwa na kazi kubwa kuhakikisha kuwa"Projection" ya dira ya Maendeleo ya Serikali ya awamu ya tano inafikiwa. 


Bunge la Bajeti la mwaka ujao linatakiwa kuwaonyesha Watanzania uwezo wao kwa kutunga Sheria nzuri za kuiwezesha Serikali kuongeza wigo wa mapato na shughuli za kiuchumi"Revenue & Economic activities Diversification".


Umahili wa kina Deo Mwanjika,Mbunge wa Njombe, Charles Kimei,Mbunge wa Vunjo,David Kihenzile,Mufundi Kusini na wabobevu wengine wengi unapaswa kuonekana hapa.


Serikali ya awamu ya tano tayari imetekeleza wajibu wake kwa kiasi fulani wa kutanua Uchumi"Widening Economic Base" kwahiyo wajibu wa Bunge ni kusaidia kubuni mipango ya kimapato kutokana na kutanuka kwa Uchumi.


Wabunge waelewe kuwa kuongeza wigo wa mapato ya Serikali kutawasidia wao pia kwani Serikali itaweza Kutimiza wajibu wake wa kutoa huduma kwa watu"Service derivery" hivyo kugusa ahadi zao walizozitoa majimboni na hiyo ndio salama yao 2025.


Bunge la kumi sio tu kwamba lina wajibu wa kubuni vyanzo vipya vya mapato"Revenue Diversification" bali pia lina wajibu wa kuhakikisha vyanzo vipya vya mapato ya Serikali vinakuwa stahimilifu"Revenue Stability".


Kwa mujibu wa Wataalam wa fedha za Umma"Public finance",ustahimilifu wa mapato ya Serikali una faida kubwa kuu mbili;kwanza kuwezesha utoaji huduma kwa wingi,wakati na kwa viwango lakini pili ustahimilifu wa mapato ya Serikali unaongeza kuaminika kwa mazingira ya biashara hivyo kuongeza Uwekezaji wa Nje.


Bunge la kumi linapaswa kuja na hoja ya kuishauri Serikali kuanzisha mfuko wa tahadhari wa kibajeti"Budget Stabilization Fund" ili kuiwezesha Serikali kuepuka kwenda kukopa katika mabenki ya kibiashara wakati wa matatizo ya majanga ya kuichumi.


Mfuko huu wa "Budget Stabilization Fund" unapaswa kutengewa fedha na fedha hizo kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Lakini mfuko huu utategemea sana uwezo na wigo wa makusanyo ya Serikali kwa kiasi gani umetanuka na umekuwa stahimilifu"Diversified and Stable".


Itoshe kusema,Bunge la kumi na mbili hakikuja kwa bahati mbaya kwani limejaa watu weledi,wana taalum nguli na watu wabobezi katika maeneo mbalimbali ya Maendeleo.


Tanzania mpya inakuja Kama sio leo basi kesho,"Just Play Your Part,It Can be Done".


+255759929244

William Peter Ndilla 

Sumve, Mwanza.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: