Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika.

Na Kadama Malunde 
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika amefungua Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) likiongozwa na Kauli Mbiu “Miaka 25 ya Beijing : Tusherehekee, Tutafakari, Tujipange, Tusonge Mbele, Twende pamoja”

Tamasha hilo litakalodumu kwa muda wa siku tatu linalofanyika katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya limekutanisha wadau wa haki za wanawake na watoto zaidi ya 300 kutoka mikoa 9 nchini ambayo ni Shinyanga, Mara, Tanga, Dar es salaam, Mbeya,Kilimanjaro,Dodoma, Mtwara na Kigoma. 

Akifungua Tamasha hilo lililohudhuriwa pia na Chifu wa Kabila la Wasafwa, Roketi Mwanshinga leo Jumatano Novemba 18,2020, Kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Mhe. William Paul Ntinika ameushukuru na kuupongeza Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kuandaa tamasha hilo. 

Ntinika alisema serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa watu wanaojihusisha na matukio ya ukatili wa kijinsia yakiwemo ya ubakaji na kuwapa ujauzito watoto. 

 "Matukio ya ukatili wa kijinsia hayana nafasi Mbeya. Tumejipanga kikamilifu ili kuhakikisha wahusika wa matukio ya ukatili wanachukuliwa hatua. Tunashukuru pia madawati ya jinsia na watoto yanafanya kazi nzuri. Mbeya ipo salama",alisema.

Aidha aliipongeza halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa kuandaa bajeti kwa mrengo wa kijinsia huku akizitaka halmashauri zingine za wilaya kutenga bajeti kwa kuzingatia makundi mbalimbali katika jamii wakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. 

“Halmashauri za wilaya zitenge bajeti kwa mrengo wa kijinsia ili kubeba sauti za watu wote katika jamii ili kujenga jamii yenye usawa”,alisema Ntinika. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi alisema tamasha hilo la Jinsia ngazi ya wilaya ni jukwaa la wazi kwa vikundi vya kijamii, vituo vya taarifa na maarifa, asasi za kiraia,taasisi za kiimani, watu binafsi na mashirika ngazi ya wilaya na mkoa kukaa pamoja na kushirikishana uzoefu,maarifa, kusherehekea mafanikio na kutafakari changamoto zilizoibuliwa katika mchakato wa mzunguko wa ujenzi wa vuguvugu la ukombozi wa wanawake kuleta usawa wa kijinsia. 

“Kauli mbiu ya Tamasha hili ni Miaka 25 ya Beijing : Tusherehekee, Tutafakari, Tujipange, Tusonge Mbele, Twende pamoja. Kupitia kauli mbiu hii washiriki watatafakari kwa kina miaka 25 ya Beijing,tulikotoka,tulipo sasa na kuweka mikakati ya kushirikisha rika zote namna ya kutathmini utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa Beijing katika kuhakikisha rasilimali zinatengwa ili kutekeleza mpango kazi wa Beijing katika ngazi zote. Tunataka Beijing iwe Kinyumbani zaidi”,alifafanua Liundi. 

Alisema ili kupata maendeleo ya haraka zaidi ni vyema wanaume na wanawake wakashirikiana kugawana fursa kwa usawa kulingana na mahitaji ya kila kundi huku akisisitia umuhimu wa kushirikisha wanawake katika ngazi za maamuzi ili changamoto za makundi mbalimbali ziingizwe katika michakato ya maendeleo. 

“TGNP imeamua kuungana na wadau wengine kuanzisha harakati za usawa wa kijinsia na haki za wanawake na jamii pamoja na kudai mgawanyo ulio sawa na wa haki wa rasilimali za taifa letu ili kutetea bajeti kwa mrengo wa kijinsia”,alisema Liundi. 

Alisema kupitia tamasha hilo la siku tatu washiriki watajadili masuala mbalimbali ikiwemo Uandaaji wa bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa ujenzi wa TAPO, Wanawake na Uongozi,Ukatili wa kijinsia,Haki ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi na mtoto wa kike, teknolojia na ubunifu. 

Naye Mjumbe Bodi wa TGNP, Jovita Mlay Tamasha la ngazi ya wilaya linafanyika kila baada ya mwaka mmoja ambapo TGNP kwa kushirikiana na vituo vya taarifa na maarifa wameshaandaa matamasha matano la kwanza lilikuwa wilayani Kisarawe mwaka 2010 likafuata la Wilayani Morogoro mwaka 2012, mwaka 2014 likafanyikia wilayani Tarime mkoani Mara na mwaka 2016 likafanyikatena wilayani Morogoro la tano lilifanyika Kishapu Shinyanga. 

Alisema kama sehemu ya Tamasha, TGNP pia imeandaa maonesho yenye lengo la kubadilisha maisha ya wanawake na vijana na mikakati ya vituo vya taarifa na maarifa katika kuimarisha vuguvugu la ukombozi wa wanawake. Kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Maonesho ya Ujenzi wa Nguvu za pamoja na Miaka 25 ya Harakati”. 

“Kwa maana hiyo washiriki wa tamasha hili wataweza kujifunza na kwa umoja wao wa kirudi katika maeneo yao wataweza kuboresha kilimo chao kwa kuanzisha mashine /viwanda vidogo vidogo au kutumia vifaa vitakavyo rahisisha maisha yao na kuwainua kiuchumi na kwa upande wa vituo vya taarifa na maarifa, kujifunza kutoka kwa wenzao mbinu zinazofanya vizuri katika kuimarisha vuguvugu katika maeneo yao”,aliongeza. 

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akisalimiana na Mkurugenzi wa Mtandao Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi baada ya kuwasili katika uwanja wa kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa ajili ya kufungua Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo Jumatano Novemba 18,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akisalimiana na Chifu wa Kabila la Wasafwa Roketi Masoko Mwanshinga baada ya kuwasili katika uwanja wa kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa ajili ya kufungua Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akifungua Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya ya Mbeya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Kulia ni Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Mbeya, Oliver Oliver Kibona 
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akifungua Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya ya Mbeya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya TGNP, Jovita Mlay akifuatiwa na Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Mbeya, Oliver Oliver Kibona akifuatiwa na Chifu wa Kabila la Wasafwa Roketi Masoko Mwanshinga.
Meza kuu wakiwa kwenye Tamasha la 6 la Jinsia wilaya ya Mbeya 2020.
Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza kwenye Tamasha la 6 la Jinsia ngazi ya wilaya lililofanyika katika uwanja wa kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

Chifu wa Kabila la Wasafwa mkoa wa Mbeya Roketi Masoko Mwanshinga akizungumza kwenye Tamasha la 6 la Jinsia ngazi ya wilaya lililofanyika katika uwanja wa kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

Mjumbe wa Bodi TGNP, Jovita Mlay akizungumza kwenye Tamasha la 6 la Jinsia ngazi ya wilaya lililofanyika katika uwanja wa kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mwakilishi wa jamii, Bi. Talaka Nyanja akizungumza kwenye Tamasha la 6 la Jinsia ngazi ya wilaya lililofanyika katika uwanja wa kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Wanawake na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akizungumza kwenye Tamasha la 6 la Jinsia ngazi ya wilaya lililofanyika katika uwanja wa kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius Temba akizungumza kwenye tamasha la sita la jinsia wilaya ya Mbeya 2020
Chifu wa Kabila la Wasafwa mkoa wa Mbeya Roketi Masoko Mwanshinga akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi (kulia).
Msanii wa nyimbo za Asili Awilo (kushoto) akitoa burudani katika tamasha la sita la jinsia wilayani Mbeya
Msanii Awilo akiendelea kutoa burudani
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akicheza wimbo wa asili wa Msanii wa nyimbo za asili Awilo baada ya kufungua Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya ya Mbeya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). 
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika , meza kuu wakipiga picha ya pamoja baada ya kufungua tamasha la 6 la jinsia ngazi ya wilaya ya Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika , meza kuu wakipiga picha ya pamoja madiwani wateule na waliokuwa madiwani wilayani Mbeya waliohudhuria tamasha la 6 la jinsia ngazi ya wilaya ya Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika , meza kuu wakipiga picha ya pamoja na maafisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri za wilaya waliohudhuria tamasha la 6 la jinsia ngazi ya wilaya ya Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika , meza kuu wakipiga picha ya pamoja viongozi mbalimbali wa kata ya Ijombe waliohudhuria tamasha la 6 la jinsia ngazi ya wilaya ya Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akiwa katika banda la TGNP kwenye maonesho yenye lengo la kubadilisha maisha ya wanawake na vijana na mikakati ya vituo vya taarifa na maarifa katika kuimarisha vuguvugu la ukombozi wa wanawake. Kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Maonesho ya Ujenzi wa Nguvu za pamoja na Miaka 25 ya Harakati”. 

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akiendelea kutembelea mabanda kwenye maonesho yenye lengo la kubadilisha maisha ya wanawake na vijana na mikakati ya vituo vya taarifa na maarifa katika kuimarisha vuguvugu la ukombozi wa wanawake. Kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Maonesho ya Ujenzi wa Nguvu za pamoja na Miaka 25 ya Harakati”. 

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akiendelea kutembelea mabanda kwenye maonesho yenye lengo la kubadilisha maisha ya wanawake na vijana na mikakati ya vituo vya taarifa na maarifa katika kuimarisha vuguvugu la ukombozi wa wanawake. 

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akiwa katika banda la Kituo cha Taarifa na maarifa Kipunguni kwenye maonesho yenye lengo la kubadilisha maisha ya wanawake na vijana na mikakati ya vituo vya taarifa na maarifa katika kuimarisha vuguvugu la ukombozi wa wanawake. 
Machifu na wadau wakipiga picha ya kumbukumbu.
Awali Maafisa Maendeleo ya Jamii halmashauri mbalimbali wakijitambulisha.
Awali Wanavituo vya taarifa na maarifa wakijitambulisha
Awali Washiriki wa jukwaa la vijana wanawake vijana wakijitambulisha
Awali wawakilishi wa asasi zinazotetea haki za wanawake na watoto wakitambulisha. 

Mwanachama wa TGNP Subira Kidiga akiimba shairi.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa kwenye tamasha
Maafisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri mbalimbali za wilaya. Kushoto ni Joseph Swalala kutoka Kishapu mkoani Shinyanga.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: