Migogoro ya Wachimbaji wa Madini inayohusu masuala ya madini haiwezi kutatuliwa kwa matamko ya Baraza la Ardhi kwa kuwa kila sheria inatumika mahala pake. Migogoro ya namna hiyo hutatuliwa kwa kuzingatia kwanza matakwa ya Sheria ya Madini.
Hayo
yamesemwa leo Novemba 20, 2020 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof.
Simon Msanjila alipotembelea eneo la mgogoro wa wachimbaji wadogo kati
ya vikundi vya Wachimbaji wadogo wa Mwime na Isalenge katika mkoa
Shinyanga Wilayani Kahama.
Mgogoro
huo kati ya vikundi hivyo, uliibuka baada ya vikundi hivyo viwili
kutofautiana wakati wakigombea kuteuliwa na Tume ya Madini kusimamia
eneo la mlipuko wa madini ya dhahau (gold rush) la Mwime wilayani
Kahama.
Katika
mchakato wa kumpata atakayepewa jukumu hilo la usimamizi, kamati
iliyoteuwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringa Macha ilikipa ushindi
kikundi cha Isalenge baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa. Kamati hiyo
ilikuwa na makundi mbalimbali kutoka katika ofisi ya wilaya na Ofisi ya
Tume ya Madini ya wilaya.
Kutoka
na maamuzi hayo Kikundi cha Mwime hakikuridhia Kikundi cha Isalenge
kupewa kazi hiyo ndipo walikwenda kushitaki kwenye Baraza la Ardhi la
Wilaya. Baraza hilo lilitoa tamko la kutengua maamuzi ya Kamati ya Mkuu
wa Wilaya kwa kufuata matakwa ya Sheria ya Ardhi.
“Kamati
hii haikuwa na upendeleo. Hoja iliyotumika kukipa ushindi kikundi cha
Iselange ni kutoka na kukidhi vigezo vilivyopangwa” alisema Macha.
Baada
ya Baraza la Ardhi kutengua maamuzi ya kamati ya Mkuu wa Wilaya, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Madini aliesema maamuzi ya Baraza la Ardhi hayawezi
kutatua mgogoro huo kwa sababu sheria za Ardhi haziingiliani na sheria
za Madini na kwamba maagizo hayo hayawezi kutekelezwa.
“Baraza
la Ardhi halina mamlaka ya kutatua mgogoro wa Wachimbaji wadogo
unaohusu masuala ya kimadini. Agizo la Baraza la Ardhi ni batili na
halitekelezeki” alisema Prof. Msanjila.
Aliongeza kuwa maamuzi ya kamati ya Mkuu wa Wilaya na maamuzi yake yataendelea kutekelezwa na sio maamuzi ya Baraza la Ardhi.
Akizunguzia
baadhi ya wachimbaji wadogo Herman Masamaki alisema mgogoro huo
unawapelekea watu kutishiwa maisha na baadhi ya watu ambao wanao onekana
kuongeaongea kwa viongozi. Alimuomba Katibu Mkuu kutoa muongozo wa
utatuaji wa mgogoro huo.
Mwajuma
Ramadhani alisema kuna tatizo juu ya utoaji wa marabaha tunatoa mifuko
mitano na mwingine anakuja kutoza tena mifuko mingine.
“Mimi
kwakweli sielewi kabisa kunamtu anakuja kutoza mrahaba badae anakuja
mwingine anatutoza tena mifuko mingine sasa hapa sielewi” alisema
Mwajuma.
Prof.
Msanjila alisema kuhusu usimamizi wa mtu au kikundi anaekusanya mapato
hapaswi kuwa mtu anaechimba katika eneo hili ndiovyo sheria inavyosema
kamati ilizingatia hili katika kuteua.
Kuhusu mrabaha alisema msimamizi hana mamlaka ya kukusanya mapato bali kusimamia eneo la machimbo na kutoa taarifa sahihi kwa mamlaka zinazohusika ili ziweze kufika na kufanya kazi yao. Asiehusika hawapaswi kukusanya mrabaha na hawapaswi kupewa.
Post A Comment: